Makala mpya

Dhamini kazi yetu

NI NINI MTAZAMO WA UISLAMU KUHUSU USHOGA?

NI NINI MTAZAMO WA UISLAMU KUHUSU USHOGA?
Ushoga: ni; Msamiati uliotumika katika kila njia za mazoea ya ngono kinyume na silika ya mwanadamu aliyoumbiwa na Mwenyezi Mungu mtukufu. Sheria ya Uislamu hulitazama jambo hilo kwa mtazamo wa kuwa ni njia mbaya, na hali za kimaradhi yasiyokuwa ya kawaida, aidha ni tabia inayochukiza ya kinyume na maumbile ya mwanadamu iliyokuwa salama, pia Shoga huhesabika kuwa ni mwenye kumuasi M/Mungu mtukufu hivyo; anastahiki adhabu ya Mungu Duniani na Akhera iwapo hatotubia makosa yake kwa Allah mwenye kusamehe na mwingi wa rehema, na hiyo ni kwa sababu Shoga huhesabika tena kuwa ni adui na dhalimu aliyechupa mipaka ya Mwenyezi Mungu. Anasema Allah katika Surat al muuminun, Aya 5-7:  ﴿وَالَّذِينَ هُمْ لِفُرُوجِهِمْ حَافِظُونَ.  إِلَّا عَلَى أَزْوَاجِهِمْ أوْ مَا مَلَكَتْ أَيْمَان ...

UHARAMU WA PUNYETO.

UHARAMU WA PUNYETO.
UHARAMU WA PUNYETO. Kujikimu mahitaji ya kijinsia kwa kutumia njia mbalimbali na kutoa manii ni jambo tumekwisha lizungumzia hapo mwanzo kuwa ni miongoni mwa madhambi makubwa, jambo ambalo Uislamu umelipiga vita. Hivyo basi ni lazima ifahamike kwamba punyeto ni sawa na mtu kujioa yeye mwenyewe kwa kumwaga maji ya uzazi kutumia mkono, ambapo kitendo hicho kimegawanyika katika aina kadhaa; Mfano kujichezea kwa mkono. Kusikiliza maongezi au sauti za Wanawake ajnabi kiasi kwamba ikapelekea kufanya kitendo hicho. Kujadiliana kuhusiana na maswala ya kimapenzi. Kuvuta taswira yale yanayosisimua hisia za matamanio ya kijinsia. Hivyo yeyote atakayekusudia kutenda kitendo cha kutoa manii kwa mkono kwa hiari yake mwenyewe, basi atakuwa ametenda dhambi kubwa ambayo kwa mujibu wa Dini tukufu ya Kiislamu ni haramu. UHARAMU WA PUNYETO KWA MUJIBU WA QUR’ANI "وَ ال ...

NI IPI HIJABU YA KISHERIA ILIYOKAMILIKA?

NI IPI HIJABU YA KISHERIA ILIYOKAMILIKA?
Hijabu (Stara) ya kisheria ziko aina mbili: Ya dhahiri na dhati. Ama hijabu ya dhahiri: ni ile hijabu ambayo Mwenyezi Mungu amewaamuru wasichana na wanawake kujihimiza kufuatilia wasifa wake, kama vile kusitiri miili yao mbele ya wanaume ajinabi na wasio waume zao, ameamrisha hilo katika Qur’ani tukufu, na kuthibitishwa na maneno ya Mtume Mtukufu (s.a.w.w) na Maimamu masumiin (a.s). Aidha maulamaa wa fiqhi wamepambanua Zaidi suala hilo, na sisi twaliashiria kwa muhtasari. Wajibu wa kuvaa hijabu ni; Msichana au mwanamke kusitiri viungo vyake kiukamilifu, ila isipokuwa uso na mikono yake kwa wasiokuwa waume zao na ajinabi, na si maalumu kwa juba pekee ila vazi linalositiri mwili kamili kwa wengine na kutotamanisha maumbile yake. Naama yampasa atakaye kujistiri kuzingatia wasifa zifuatazo: Asiwe anavutia. Asiwe amevaa mavazi yanayombana (yana ...

JE! WAKE WENGI NI MITALA INAYOTEGEMEA UHAKIKA WA UADILIFU WAO?

JE! WAKE WENGI NI MITALA INAYOTEGEMEA UHAKIKA WA UADILIFU WAO?
Swali: Nini mtazamo Kiislamu juu ya haki za kifamilia? Je! Kuongeza wake ni mitala inayotegemea uhakika wa uadilifu wao? Jawabu: Ndiyo, Hakika hayo hutegemea uaminifu wa mtu mwenyewe kufikia uadilifu baina ya wakeze. Anasema Mwenyezi Mungu katika Surat Anisaai: 3: (وَإِنْ خِفْتُمْ أَلَّا تُقْسِطُوا فِي الْيَتَامَىٰ فَانكِحُوا مَا طَابَ لَكُم مِّنَ النِّسَاءِ مَثْنَىٰ وَثُلَاثَ وَرُبَاعَ فَإِنْ خِفْتُمْ أَلَّا تَعْدِلُوا فَوَاحِدَةً). “Na ikiwa mnaogopa kuwa hamtowafanyia mayatima uadilifu, basi oeni mnao wapenda katika wanawake, wawili au watatu au wane. Na mkiogopa kuwa hamwezi kufanya uadilifu, basi mmoja tu”. Hakika wanachuoni wetu wameeleza kwa ubainifu zaidi katika vitabu vya kifiqhi na risala z ...

KUHUSU BAADHI YA MISIMAMO KWA MWANAMKE:

KUHUSU BAADHI YA MISIMAMO KWA MWANAMKE:
Swali: Uislamu hakutofautisha katika kuwaagiza kidini kati ya wanaume na wanawake, wote wawili wako sawa katika matilaba kuhusu kumuabudu Mungu, kusimamisha Dini yake na kulingania watu kumuelekea Allah, kuamrisha mema na kukemea mabaya. Aidha Qur’ani imembebesha Mwanamume na Mwanamke majukumu ya kusimamia masilahi ya jamii na kuurekebisha- kwa maana kwamba kuamrisha mema na kukemea mabaya- katika kauli ya Mwenyezi Mungu: (وَالْمُؤْمِنُونَ وَالْمُؤْمِنَاتُ بَعْضُهُمْ أَوْلِيَاءُ بَعْضٍ يَأْمُرُونَ بِالْمَعْرُوفِ وَيَنْهَوْنَ عَنِ الْمُنكَرِ وَيُقِيمُونَ الصَّلَاةَ وَيُؤْتُونَ الزَّكَاةَ وَيُطِيعُونَ اللَّـهَ وَرَسُولَهُ). “Na Waumini wanaume na Waumini wanawake wao kwa ...

DHAMBI YA KULAWITI

DHAMBI YA KULAWITI
NINI MAANA YA LIWAAT? Bila shaka kitendo cha kulawiti ni kitendo kibaya mno chenye kuchukiza, hivyo ni wazi kwamba yeyote anayetenda dhambi hiyo, basi ni dalili ya uchache wa akili zake, na  hutubainishia ya kwamba dhamira ya mtu huyo imekwisha pigwa muhuri wa kila ovu. Ambapo dhati yake mwenyewe haitulii ila kwa kutenda kitendo hicho cha haramu na ili atulize matamanio kupitia uchafu huu. Hakika kitendo cha kulawiti ni dhambi nzito mno, kama vile dhambi iliyopelekea Kaumu ya Nabii Luut kuangamia kwa adhabu kali. Mwenyezi Mungu anasema katika Qur’ani tukufu, Surat Ashuaa’raa, Aya ya 165-166, anahutubia kwa kuwakaripia kaumu ya watu mfano wa hao: "أَتَأْتُونَ الذُّكْرَانَ مِنَ الْعَالَمِينَ * وَتَذَرُونَ مَا خَلَقَ لَكُمْ رَبُّكُمْ مِنْ أَزْوَاجِكُم بَلْ أَ ...

JE,INAJUZU MUME KUTOA TALAKA TATU KWA MARA MOJA?

JE,INAJUZU MUME KUTOA TALAKA TATU KWA MARA MOJA?
Ndugu zangu waislaam:—Assalam Alaikum—Kwanza kabisa tuna kila 7babu ya kumshukuru muuliza swali kwa kuuliza swali zuri na muhimu kama hili,na hapo ndipo tunapokumbuka msemo huu usemao:((Swali au kuuliza ni nusu ya elimu)).Na tunaweza kuchangia ktk kujibu swali hili kama ifuatavyo: Kama tunavyojua na kufahamu,Mwenyeezi Mungu (s.w) kamuumba Mwanadamu akiwa ni mtu wa kijamii kisha akayafanya Maisha yake kuwa ni maisha yaliyojaa bahati na utulivu.Hivyo Mwanadamu kuwa pamoja na Jamii na kuishi Maisha ya Kijamii ni moja kati ya mambo muhimu na ya msingi anayo yahitajia mno Mwanadamu,kutokana na hilo tunamkuta Allah (s.w) katika Qur’an Tukufu na Mtume wake (s.a.w.w) katika Sunna Tukufu wakituwekea utaratibu na kanuni bora zinazohitajika katika maisha salama ya mwandamu ili tuweze kuishi au kuwa na maisha bora ya kifamilia,maisha ya utulivu,yenye wingi wa s ...

Falsafa ya Mwezi Mtukufu wa Ramadhan

Falsafa ya Mwezi Mtukufu wa Ramadhan
Sifa zote njema ni za Mwenyeezi Mungu,Mola Mlezi wa viumbe vyote.Na sala na salam ziwe kwa mwenye kubashiri na kuonya ambaye ni taa yenye kuangaza,Bwana wetu na Nabii wetu Muhammad (s.a.w.w) na Ahli zake Muhammad,ambao ni bora,ni watwaharifu na ni Maasumin (a.s).Laana zote ziwe juu ya wale wote ambao ni maadui wao,kuanzia sasa mpaka itakaposimama siku ya kiyama. Maudhui yetu itakuwa ni:Umuhimu wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhan na kujikurubisha zaidi ndani ya mwezi huu kwa Allah (s.w): Mwenyeezi Mungu (s.w) amesema: (شَهْرُ رَمَضانَ الَّذی أُنْزِلَ فیهِ الْقُرْآنُ هُدىً لِلنَّاسِ وَ بَیِّناتٍ مِنَ الْهُدى‏ وَ الْفُرْقان) “Mwezi wa Ramadhani ambao imeteremshwa ndani yake Qur’an kuwa mwongozo kwa watu,na hoja zilizo wazi za uwongofu na upambanuzi.” Suratul-Baqara ...

Wasiliana nasi | RSS | Ramani ya Tovuti

Haki zote za Tovuti hii Islam 14 zimehifadhiwa,hivyo inaruhusiwa kutumia makala yoyote ya tovuti hii sambamba na kutaja chanzo chake.