Makala mpya

Dhamini kazi yetu

FADAK KATIKA UISLAM

rp_Fadak.gif

SEHEMU YA 2

 Katika sehemu ya kwanza tulitoa muhtasari kuhusiana na mjadala huu au maudhui hii.Muhtasari huo ulikuwa katika mfumo wa maswali muhimu yanayoulizwa kuhusiana na kadhia ya Fadak.

Tukasema nini maana ya Fadak na ilitoka wapi hiyo Fadak?.Na nukta zingine muhimu ambazo zote zimejengeka katika msingi wa maswali.

Sehemu hii na sehemu zingine zijazo -Insha Allah- tutatajaribu kufafanua kwa upana zaidi nukta hizo na kubainisha maswali hayo kama ifuatavyo:

Fadak: Ni neno la Kiarabu ambapo katika sehemu iliyopita tuliashiria katika maana ya Fadak tukisema kwamba Fadak:Ni shamba au Bustan au (Ardhi ya Kilimo) iliyokuwa karibu na eneo linaloitwa Khaybar,lililopo Kaskasizi mwa Hijaz ambapo leo hii eneo hilo limekuwa ni sehemu ya Saudia Arabia.Masafa yaliyopo kutoka Mji Mtukufu wa Madina hadi eneo hilo ni Takriban kilomita 100.

Fadak hiyo (au Ardhi hiyo) ilijulikana  sana kwa sababu ilikuwa ni Ardhi safi iliyokuwa na visima vya maji,mitende,na kazi za mikono.

Fadak ilikuwa ni mali ya Mayahudi waliokuwa wakiishi Hijaz ambapo walikuwa wakimiliki ardhi kadhaa,moja ya ardhi hizo ilikuwa ni Khaybar na nyingine ilikuwa ni Fadak.

Tunajua kwamba Uislam ulipoanza katika Mji Mtukufu wa Makka na baadae Mtume (s.a.w.w) kuhamia katika mji wa Madina ulikuwa na idadi kubwa ya maadui kiasi kwamba ukakumbwa na vita kadhaa na ukakabiliana na vita hivyo.

Mayahudi walikuwa ni sehemu ya maadui hao wa Uislam ambapo waliibua vita dhidi ya Uislam.Hatimae Mtume (s.a.w.w) akatoa amri ya kukabiliana kivita na maadui hao wa Kiyahudi.

Moja ya vita hivyo dhidi ya Mayahudi hao ilikuwa ni vita vya kihistoria vya Khaybar, ambapo vita hiyo inadhihirisha  sifa ya pekee katika uwanja wa kivita na ushujaa mkubwa wa aliokuwa nao Amirul-Muuminina Al-Imam Ali bin Abi Talib (a.s).

Jeshi la Waislam wakiongozwa na Amirul-Muuminina Ali bin Abi Talib (a.s) walielekea huko Khaybar kukabiliana na Mayahudi hao azma yao ikiwa ni moja tu kupata ushindi na eneo hilo kuwa chini ya Uislam.Tukumbuke kwamba “Khaybar” lilikuwa  ni eneo muhimu sana la kiistratejia la Mayahudi.

Katika vita hiyo Waislam wakapata ushindi na kuimiliki Khaybar.Mayahudi wote wakapata khabari ya kwamba eneo lao muhimu sana la Khaybar sasa limetekwa na lipo mikononi mwa Waislam.

Hivyo Mayahudi  hao wakashauriana kwamba ikiwa tutataka kupambana na Muhammad (s.a.w.w) na kuleta upinzani dhidi yake,basi hakuna shaka kuwa tutapoteza mali zetu zote,ardhi zetu na hata nafsi zetu.

Hivyo itakuwa ni bora zaidi tukijisalimisha kwake bila kufanya vita yoyote dhidi yake.

Hivyo moja ya Ardhi za Mayahudi zilizoingia katika milki au mikononi mwa Waislam kwa amani bila kupitia vita ilikuwa ni Ardhi ya Fadak, ambapo Mayahudi baada ya kushindwa katika vita hiyo ya Khaybar,waliamua kujisalimisha kwa Mtume (s.a.w.w) na kusitisha vita dhidi ya Uislam.

Na ili kudhihirisha kuwa wanasitisha Muqawamah na upinzani wao dhidi ya Mtume (s.a.w.w) wakaamua kumpatia Mtume (s.a.w.w) Ardhi ya Fadak.

Lakini baadhi ya watu wanaitikadia au wanaamini kwamba Mayahudi hao waliamua kuachia au kumpatia Bwana Mtume (s.a.w.w) Ardhi hiyo ya Fadak wakiwa na lengo la kuzuia vita (isitokee) baina yao na Mtume (s.a.w.w),na kuwa hilo linamaanisha kwamba Fadak hiyo ilipatikana kwa njia ya vita.(Hiyo ni fikra na mawazo ya baadhi ya watu wakifafanua kuhusiana na upatikanaji wa Fadak hiyo).

Kabla ya kifo cha Bwana Mtume (s.a.w.w),Mtume (s.a.w.w) aliitoa Zawadi Fadak hiyo kwa Binti yake Fatimah Zahra (s.a) ikiwa ni urithi wake kutoka kwa Baba yake Mtume Muhammad (s.a.w.w).Hii inamaanisha kwamba Fadak ilikuwa katika milki ya Sayyidat Fatimah Zahra (s.a) wakati wa uhai wa Mtume (s.a.w.w).

Kwa ibara nyingine:Mtume (s.a.w.w),umiliki wa shamba hilo au Fadak hiyo aliuhamishia kwa Fatimah  Zahra (s.a) na hilo alilifanya Bwana Mtume (s.a.w.w) katika uhai wake kabla ya kifo chake.

Lakini pamoja na hayo,Fadak hiyo ikawa sehemu ya mgogoro na mvutano kati ya Binti ya Mtume (s.a.w.w) yaani Sayyidat Fatimah Zahra (s.a) na Khalifa Abu Bakar.

Baada ya Kifo cha Mtume (s.a.w.w),Abu Bakar akaamua kuishika Ardhi hiyo ya Fadak na kusema kuwa Mtume au Nabii “harithiwi” na kwamba Fadak hiyo baada ya kuachwa na Mtume (s.a.w.w) inakuwa mali ya waislam!.

Lakini Fatimah Zahra (s.a) Binti ya Mtume (s.a.w.w) akaamua kumfuata huyo Abu Bakar na akatoa madai yake kuwa yeye ndiye mmiliki na mrithi wa Fadak hiyo ikiwa ni mali ya Baba yake Mtume Muhammad (s.a.w.w).

Swali muhimu ni hili:Je,ni kweli kwamba Mtume (s.a.w.w) hana mrithi (kwa maana harithiwi)?.

Ni kwanini Mtume (s.a.w.w) asirithiwe hali ya kuwa Mitume wengine wanao warithi na wamerithiwa?!.

Pindi Qur’an Tukufu ilipozungumzia suala la urithi na kuandika wasia,je ilisema kuwa suala hilo halimhusu Mtume (s.a.w.w)?!.

Vyanzo vinaripoti kuwa Imam Ali (a.s) akiwa pamoja na Ummu Ayman walitoa ushahidi wao juu ya uhakika na ukweli huu kwamba:Mtume Muhammad (s.a.w.w) aliitoa zawadi Fadak hiyo kwa Fatimah Zahra (s.a).

Ushahidi huo waliutoa pale tu Abu-Bakar alipomtaka Fatimah Zahra (s.a) kuwaita Mashahidi wake ili waje kutoa ushahidi na kuthibitisha madai yake.Lakini Abu-Bakar alikataa (shahada au) ushahidi wa Imam Ali (a.s) kuhusiana na hilo na akakataa pia ushahidi wa Ummu Ayman.

Hapa ni lazima tujiulize  swali hili la kimantiki:Ikiwa kweli Nabii Muhammad (s.a.w.w) harithiwi,basi ni kwa nini Abu Bakar anaomba Ushahidi kwa Fatimah Zahra (s.a) ili kuthibitisha Madai yake?!.

Na alipoomba (Abubakar) aletewe ushahidi utakao thibitisha madai ya Fatimah Zahra (s.a),Binti wa pekee na kipenzi wa Mtume Muhammad (s.a.w.w),basi ni kwa nini alikataa (shahada au) ushahidi wa mashahidi hao walioletwa na Fatimah Zahra (s.a)?.

 Vyanzo mbalimbali na vya msingi vinathibitisha  kwamba Mtume (s.a.w.w) aliitoa Fadak hiyo kwa Binti yake Fatimah Zahra (s.a),na vinatumia (vyanzo hivo) Qur’an Tukufu kama ushahidi.

Hii ni pamoja na zile riwaya za Ibn Abbas ambapo anasimulia akisema kwamba:Iliposhuka Aya ya Qur’an Tukufu inayozungumzia kuhusiana na kuzitoa haki kwa wenye kustahiki haki hizo,Mtume Muhammad (s.a.w.w) alimuita binti yake Fatimah (s.a) na kuitoa zawadi Ardhi hiyo ya Fadak kwa Fatimah (s.a).

Wanazuoni mbalimbali wa Tafsiri ya Qur’an Tukufu wanatoa maoni yao juu ya Qur’an Tukufu (katika Aya husika) wakisema kwamba:Malaika Jibrail (a.s) alikuja kwa Mtume Muhammad (s.a.w.w) na kumuamuru kuwapa “Dhul-Qurba” (yaani: Jamaa wa karibu) haki zao.Pindi Mtume Muhammad (s.a.w.w) alipomuuliza Jibrail (a.s) kuhusiana na : “Dhul-Qurba” kwamba ni nani aliyekusudiwa au Dhul-Qurba ni nani?. Jibrail (a.s) alijibu akisema: “Fatima” na “Haki” iliyokusudiwa ilikuwa ni “Fadak”.

Na hapo ndipo Mtume Muhammad (s.a.w.w) alipomuita Fatima Zahra (s.a) na kumpatia Fadak hiyo.

Hata hivyo ni kwamba:Fatimah Zahra (s.a) kamwe hakuwa na mahitajio yoyote (maadiy) ya kimaada kwa Fadak hiyo,lakini pamoja na hayo hiyo Fadak imekuwa  mali yake binafsi ambapo hakuna mtu mwenye haki ya kumuudhi kwa kumnyang’anya mali yake na haki yake.Pia (Ira’da) au maamuzi au mapenzi ya Mtume Muhammad (s.a.w.w) yanatakiwa bali ni lazima kuheshimiwa.

Je,kukataa na kupinga (maamuzi au) mapenzi (Ira’da) ya Mtume Muhammad (s.a.w.w),vile vile kukataa shahada (au ushahidi) wa Imam Ali na Ummu Ayman si ni kitendo cha uzembe na kibri (au jeuri) kwa Mtume (s.a.w.w) na kwa wawili hawa yaani Imam Ali bin Abi Talib (a.s) na Ummu Ayman?!.

Ingawa kuchukuliwa kwa Fadak kutoka kwa Fatimah Zahra (s.a) ilikuwa ni mwendelezo wa njama na tukio zima la Saqifa Bani Saad  na kwa mujibu wa ushauri wa Omar bin Khatab kwamba Fadak hiyo hatakiwi kupewa Fatimah Zahra (s.a) na kwamba Ushahidi wa Mashahidi wa Fatima (s.a) hautakiwi kukubaliwa (kwa vyovyote vile itakavyokuwa) kwa sababu matokeo ya kukubali ushahidi wa Fatima (s.a) itakuwa ni kukubali tu (hakuna jinsi) madai yake na tutalazimika kukubali kuwa Imam Ali (a.s) ndiye Khalifa.

Hivyo ndio maana Omar bin Khatab aliamua kumpinga Abu-Bakar kwa nguvu zake zote alipotaka (Abu-Bakar) kukubali madai ya Fatimah Zahra (s.a).

To be continue

ارسال یک پاسخ

Barua pepe yako haitachapishwa.
Sehemu ya lazima imeonyeshwa kwa alama ya * .

*


Wasiliana nasi | RSS | Ramani ya Tovuti

Haki zote za Tovuti hii Islam 14 zimehifadhiwa,hivyo inaruhusiwa kutumia makala yoyote ya tovuti hii sambamba na kutaja chanzo chake.