Makala mpya

Dhamini kazi yetu

Kumuudhi Sayyidat Fatimah -s.a- ni kumuudhi Mtume -s.a.w.w

Enyi mlioamini! Ni kwa nini mnayasema msiyoyatenda.Inachukiza vikubwa mno kwa Mwenyeezi Mungu kuwa mnayasema yale msiyoyatenda.Fatima (s.a) alifanya nini Abubakar alipokataa kumrudishia Fadak yake?!.Je, Abu Bakar alihudhuria Mazishi ya Sayyidat Fatima (s.a) au la?.Kwa nini Sayyidat Fatma (s.a) alizikwa usiku na Kaburi lake halijulikani lilipo?!.

Je,ipo sehemu yoyote ndani ya sahihi Bukhari au sahihi muslim kuliponukuliwa kuwa Mtume (s.a.w.w) kuhusu Binti yake Sayyidat Fatima (s.a):”Fatima anatokana na mimi,hivyo mwenye kumuudhi  (kumghadhibisha) Fatma atakuwa ameniudhi mimi”,…..”mwenye kumfurahisha Fatima atakuwa amenifurahisha mimi”?!.
Je,Kuna sehemu yoyote katika Qur’an Tukufu alipotutaka Mwenyeezi Mungu (s.w) kuwapenda Ahlul-Bait wa Mtume (s.a.w.w) na kuwapenda ikawa ni wajibu kwetu?!.Je,inakuwaje kwa yule aliyekuwa jasirii kumdhulumu Sayyidat Fatima (s.a) haki yake na ambaye imethibiti ndani ya historia kuwa Sayyidat Fatima (s.a) alifariki katika hali ya kumghadhibikia na akausia Sayyidat asishiriki katika mazihi yake wala kujua ni wapi lilipo kaburi lake?!.Je,Sayyidat Fatima (s.a) si imethibiti katika Riwaya na Hadithi sahihi na zilizopo ndani ya sahihi Muslim na  Sahihi Bukhari kuwa yeye ni anatokana na Mtume (s.a.w.w) na kwamba kumuudhi yeye ni kumuudhi Mtume (s.a.w.w)?.
Na iakuwaje kwa mwenye Kumuudhi Mtume (s.a.w.w)?!.Jawabu lake lipo katika Suratul-Ahzab Aya ya 57.Aya hiyo inaweka wazi malipo ya Mtu mwenye kumuudhi Mtume wa Mwenyeezi Mungu (s.w

ارسال یک پاسخ

Barua pepe yako haitachapishwa.
Sehemu ya lazima imeonyeshwa kwa alama ya * .

*


Wasiliana nasi | RSS | Ramani ya Tovuti

Haki zote za Tovuti hii Islam 14 zimehifadhiwa,hivyo inaruhusiwa kutumia makala yoyote ya tovuti hii sambamba na kutaja chanzo chake.