Makala mpya

Dhamini kazi yetu

KWA NINI MIMI SIO MKRISTO: NI MAZUNGUMZO KATI YA UISLAM NA UKRISTO

Assalam Alaikum

Kwa mujibu wa mtazamo wa Uislam Hadhrat Maryam (s.a) ni mwanamke msafi,mtakatifu,bora na Mchamungu,zaidi ya hilo ni Mwanamke Maasum hamuasi Mwenyeezi Mungu (s.w).Hadhrat Maryam (s.w) hakuolewa kabla ya kumzaa Hadhrat Masih Isa (a.s) na baada ya kumzaa.Hadhrat Maryam (s.a) ni mwanamke bora na mfano bora wa kuigwa kwa wanawake wote.Hakujipamba na sifa mbaya za ukahaba na mengine yamchukizayo Mwenyeezi Mungu (s.w).Bi.Maryma (s.a) ni Mwanamke anayetukuzwa sana ktk Uislaam na ukichunguza ktk Qur’an hutalikuta jina la mwanamke ispokuwa jina moja tu la Hadhrat Maryam (s.a).Na si hilo tu bali Allah (s.w) amelifanya jina la Maryam (s.a) kuwa ni jina la Sura miongoni mwa Sura 114 za Quran Tukufu ambapo Sura moja kati ya hizo 114 inaitwa:Surat Maryam.
Yeye ni Mama mzazi wa Hadhrat Masih Isa (a.s) na si mama wa mungu au mama wa mtoto wa mungu!.Na Hadhrat Masih Isa bin Maryam (a.s) ni Mja miongoni mwa waja wa Mwenyeezi Mungu (s.w),yeye ana mama ana bibi na babu,hivyo si mungu wala mwana wa mungu bali yeye ni Nabii miongoni mwa Manabii wa Mwenyeezi Mungu (s.w).Uislam unawaheshimu watkufu hawa wawili yaani Hadhrat Maryam (s.a) na Hadhrat Masih (a.s) na ni dhambi kubwa ktk Uislam kuwavunjia heshima watukufu hawa na wabora mbele ya Mwenyeezi Mungu (s.w).Kama ambavyo kumtukana Mtume (s.a.w.w) na kumvunjia heshima unatoka moja kwa moja ktk Uislam na unakuwa ni kafiri uliyebayana hivyo hivyo ndivyo ilivyo kwa Hadhrat Masih (a.s) na Hadhrat Maryam (s.w).
Muislam sio Mkristo na sio mkristo kwa sababu ya kutojua chochote kuhusu ukristo bali yeye sio mkristo kwa sababu ya zile ishkali mbalimbali zinazoelekezwa ktk ile inayoitwa dini ya ukristo na dalili mbalimbali zilizopo zinazothibitisha kwamba dini ya Mwisho ni dini tukufu ya Kiislaam iliyokuja kuzifuta dini zote ma kuwaita watu wote wawe waislam na kufuata dini moja ya uislaam.Wafuasi sahihi wa Yesu Isa bin Maryam (s.w) ni wale wanaosema sisi ni WAISLAM kama walivyomjibu Hadhrat Masih (a.s) pale alipowauliza:
فَلَمَّا أَحَسَّ عِیسَى مِنْهُمُ الْکُفْرَ قَالَ مَنْ أَنصَارِی إِلَى اللّهِ قَالَ الْحَوَارِیُّونَ نَحْنُ أَنصَارُ اللّهِ آمَنَّا بِاللّهِ وَاشْهَدْ بِأَنَّا مُسْلِمُونَ
۵۲

.Alipohisi Isa ukafiri wao alisema: “Nani watakuwa wasaidizi wangu kwa Mwenyezi Mungu?” Wanafunzi wakasema:”Sisi ni wasaidizi wa Mwenyezi Mungu.Tumemwamini Mwenyezi Mungu nawe shuhudia kuwa sisi ni Waislamu
Kisha wakasema:
رَبَّنَا آمَنَّا بِمَا أَنزَلَتْ وَاتَّبَعْنَا الرَّسُولَ فَاکْتُبْنَا مَعَ الشَّاهِدِینَ
۵۳

.”Mola wetu! Tumeyaamini uliyoyateremsha, na tumemfuata Mtume, basi tuandike pamoja na washuhudiao”
Surat Aali Imran
Karibu tena
Na Taqee Zachalia

ارسال یک پاسخ

Barua pepe yako haitachapishwa.
Sehemu ya lazima imeonyeshwa kwa alama ya * .

*


Wasiliana nasi | RSS | Ramani ya Tovuti

Haki zote za Tovuti hii Islam 14 zimehifadhiwa,hivyo inaruhusiwa kutumia makala yoyote ya tovuti hii sambamba na kutaja chanzo chake.