Makala mpya

Dhamini kazi yetu

Mbingu Kulia na Kunyesha Mvua ya Damu katika Msiba Mkubwa wa Kuuliwa Imam Husein a.s

 بسم الله الرحمن الرحیم

گریه و باران خون آسمان در مصیبت اعظم

Mbingu Kulia na Kunyesha Mvua ya Damu

katika Msiba Mkubwa wa Kuuliwa Imam Husein a.s

KWA JINA LA MWENYEEZI MUNGU MWINGI WA REHEMA MWENYE KUREHEMU

السلام علیک یا ابا عبد الله اشهد ان مصیبتک اعظم المصیبه فی السماوات و الارض و علی جمیع اهل السماوات و الارض

AMANI IWE JUU YAKO EWE HUSEIN BIN ALI (ABA ABDILLAH) (A.S).NINASHUHUDIA YA KWAMBA MSIBA WAKO NI MSIBA MKUBWA (NA MZITO) KWA  MBINGU NA ARDHI NA KWA WATU WOTE WA MBINGUNI NA ARDHINI.

 

لازم به ذکر است که کتب تاریخ اروپایی  که چنین واقعه ای  را ثبت  کرده اند تنها به کتاب انگلو سکسون کرونیکل محدودو نمیگردد و از یک کتاب تجاوز میکند از این دست کتابها میتوان نام کتبی مانند ورش لتینک کرونیکل و یا کرونیکل آو پرنسیس را نام برد.

جان ودادی مستند ساز و پژوهشگر بریتانیایی توضیحات بیشتری را با ما در میان میگذارد:

Ni muhimu kuashiria katika nukta hii kwamba Vitabu vya Kihistoria vya Magharibi vilivyosajiri na kunukuu tukio hili ni vingi mno kiasi kwamba halikuishia tu kunukuliwa ndani ya Kitabu kiitwachoThe Anglo-Saxon ((SAKSON))Chronicles”,bali limenukuliwa pia katika vitabu vingine kama vile: The Welsh Latin Chronicles au The Chronicle of the Princes.

John Vedadi, Mtengenezaji wa Filamu za Documentary (Documentary Film Maker) raia wa Uingereza anatubainisha zaidi kuhusiana na maudhui hii akisema:

من در تحقیقاتم بر روی کتاب انگلو سکسون به مطلب بسیار عجیبی برخوردم در این مطلب نوشته شده است : که حدود سال ۶۸۹ میلادی در بریتانیا باران خون آمده است و کره ها و شیرها به خون تبدیل شده است .

این نوشته به تنهایی غیر عادی میباشد .ولی علاوه بر این کتاب دو کتاب تاریخی ارزشمند نیز است اولی ” ولش لتینگ گرونیکل و دومی کرونیکل اف د پرنسس و در هر دوی این کتابها همین موضوع مطرح شده است و چون سه کتاب از شمال شرق اروپا این موضوع را عنوان میکنند برای ما جلب توجه کرده و ما را وادار میکند

تا در مورد دلیل این اتفاق تحقیق کنیم .

Katika utafiti wangu kuhusiana na Kitabu kiitwacho:The Anglo-Saxon chronicles nimekumbana na jambo la ajabu sana ambapo imeandikwa ndani yake kuhusiana na jambo hilo kwamba:Mnamo mwaka 689 A.D,ilinyesha Mvua ya Damu katika nchi ya Uingereza, ambapo Maziwa pamoja na Siagi vilibadilika na kuwa damu!.

Kwa  hakika tukio hilo sio la kawaida.Hata hivyo, mbali na Kitabu hiki pia kuna vitabu vingine viwili vya Kihistoria vyenye thamani:Cha kwanza kinaitwa:

The Welsh Latin Chronicles.Na cha pili kinaitwa: The Chronicle of the Princes

Ndani ya vitabu hivi viwili pia limetajwa tukio hili,na kwa sababu ya ukweli huu kwamba Vitabu vitatu tofauti, kutoka eneo la Kaskazini Magharibi mwa Ulaya vimenukuu tukio hili,suala hilo limetustaajabisha na kutuvutia na kutufanya tuwe makini na kufanya utafiti ili kujua tukio hilo lilikuwa linahusu nini.

البته این کتابها مربوط به تاریخ قرون وسطی است .

یعنی زمانی که کلیسا حاکم بر جامعه بوده و بحث دین در این زمان امری طبیعی محسوب میشده .

اینبار به سراغ منابع علم دین مسیحیت رفتیم تا نظر آنها را نیز جویا شویم .

با مطالعه این پایگاه اینترنتی مسیحی که  به بشارات کتاب مقدس پرداخته بود بعضی وقایع را به عنوان عذاب الهی معرفی کرده و آنها را نام برده که از جمله این وقایع باران خونی که در سال ۶۸۵ میلادی در کشورهای اروپا باریده و آن را یک عذاب الهی معرفی کرده است .

(MSIMULIZI):Bila shaka vitabu hivi vinahusiana na Historia ya Zama za Kati (Medieval History),yaani zama zile ambazo,Kanisa lilikuwa likitawala Jamii,na majadiliano ya kidini katika zama hizo lilikuwa likihesabika kuwa ni jambo la kawaida.

Wakati huu,tumeamua kwenda katika vyanzo vya kielimu vya Dini ya Ukristo ili pia tuweze kuwauliza juu ya maoni yao.

Kwa kusoma Tovuti hii ya Kikristo iliyokuwa ikitoa Bishara (au Masomo) ya Biblia,tunaikuta inayabainisha baadhi ya matukio kwa anuani ya Adhabu ya Mwenyezi Mungu,na imeyataja matukio hayo, ambayo ni pamoja na tukio hili la kunyesha Mvua ya Damu, lililotokea mwaka 685 A.D katika nchi za Ulaya,na tukio hilo limetajwa katika Tovuti hiyo katika anuani ya kuwa ni Adhabu ya Mwenyeezi Mungu.

چگونه میتوان با وجود خفقان و محدودیتهای قرون وسطی مطالب ثبت شده در آن دوره تاریخی را به عنوان سند تاریخی پذیرفت .

این سوء ظن ما را بر آن داشت تا سری به اسناد تاریخی بزرگترین و معتبر ترین تمدن آن زمان بزنیم : اسلام .

اشهد ان علیا حجه الله ….

(MSIMULIZI):Katika mazingira ya kuwepo hali ya ukandamizaji na vizuizi katika Zama za Kati,utawezaje kukubali mambo yaliyothibiti katika kipindi hicho cha Kihistoria, kwa anuani ya Hati ya Kihistoria?!.

Dhana yetu mbaya kuhusu hilo, imetufanya tuelekee katika nyaraka kubwa za Kihistoria na zenye itibari zaidi katika Ustaarabu wa Zama hizo:  Uislaam:

Nina Shuhudia ya kwamba Ali ni Hoja wa Mwenyeezi Mungu……

گوستاو لیبون مورخ و جامعه شناس قرن نوزده فرانسوی میگوید تا قرن پانزده میلادی دانشمندان گفته ای را که از دانشمندان مسلمان اخذ نشده بود تایید نمیکردند.

دوران شکوفایی اسلام یکی از برجسته ترین و بزرگترین تمدنها دقیقا مقارن با قرون وسطی بوده و جالب اینکه کتب تاریخی این تمدن بزرگ نیز چنین واقعه ای یعنی باران خون را در حدود همان سال ، سال ۶۸۵  میلادی در مناطق مختلف جغرافیایی همچون روم ، عراق ایران ، یمن و مناطق دیگر گزارش کرده اند و یا تایید کرده اند .

برای این مهم به سراغ متخصصین تاریخ تمدن اسلامی در نقاط مختلف دنیا رفتیم تا شاید با توضیحات ایشان بتوانیم نقطه وصلی بین این گزارشات و گزارشهای ثبت شده در تاریخ اروپا پیدا کنیم .

 

(MSIMULIZI):Gustave Le Bon Mwanahistoria na Mwanasosholojia wa Ufaransa wa karne ya 19 anasema:

Mpaka karne ya 15 A.D,kauli yoyote ile ambayo ilikuwa haijachukuliwa toka kwa Wanazuoni wa Kiislam,basi Wanazuoni walikuwa hawaithibitishi.

Kustawi kwa Uislamu hasa kuelekea katika Zama za Kati ilikuwa ni moja ya Ustaarabu maarufu na mkubwa zaidi,na jambo la kuvutia zaidi ni kwamba Vitabu vya Kihistoria vya Ustaarabu huu mkubwa wa Kiislaam pia vimelitaja au kulithibitisha tukio hili,yaani tukio la Kunyesha Mvua ya Damu lililotokea mwaka 685 A.D katika maeneo tofauti ya kijiografia kama vile:Roma,Iraq,Iran,Yemen,….na maeneo mengine tofauti na hayo.

Kwa ajili ya tukio hili muhimu, tuliamua kwenda kwa Wataalam wa Ustaarabu wa Kiislamu katika sehemu mbalimbali za Dunia,ili huenda kupitia maelezo yao na ufafanuzi wao tukaweza kuipata nukta inayoziunganisha ripoti mbili,yaani:Ripoti tutakazozipata toka kwa Wataalamu hao na zile Ripoti zilizothibiti katika vitabu vya Kihistoria vya Ulaya.

ذکر شده که در شام و حجاز و خراسان و بیت المقدس باران خون دیده شد.

Imetajwa kwamba Mvua ya Damu ilishuhudiwa katika maeneo ya Sham,Hijaz,Khurasan,na Baitul-Maqdis.

در یکی از معتبر ترین کتب اهل سنت با نام بغیه الطلب فی تاریخ حلب از شخصی به نام جعفر بن سلیمان اینگونه مینویسد : آنقدر باران خون آمد که اثر آن تا مدتها بر در و دیوار منزل مانده بود و آنها خونی شده بودند .

باران خون به بصره کوفه شام و خراسان نیز رسید و شک نداشتیم که به زودی عذابی نازل خواهد شد .

(MSIMULIZI):Katika moja ya vitabu vya Kisunni vyenye itibari kubwa kinachoitwa:Bughiyyatut-Talab Fi Tarikhi Halab,yameandikwa ndani yake yafuatayo kutoka kwa mtu anayeitwa Jaafar bin Suleiman:

“Ilinyesha Mvua kubwa ya Damu kiasi kwamba athari ya mvua hiyo ikabaki juu ya milango na kuta za nyumba kwa muda mrefu,kiasi kwamba milango na kuta hizo zikawa za damu.

Mvua ya Damu ikafika Basra,Kuufa,Sham,na Khurasani,na hatukuwa na shaka kwamba hivi karibuni Adhabu ya Mwenyeezi Mungu itashuka”.

در منابع اهل سنت این قضیه به صورت وسیعی گزارش شده در منابع حدیثی و تاریخی در کتاب ذخائر العقبی طبری شافعی و همینطور کتاب تاریخ دمشق ، صواعق المحرقه ، الخصائص الکبری ، ینابیع الموده ، تذکره الخواص ، سیر اعلام النبلاء ذهبی ، تاریخ الخلفاء ، کتاب احقاق الحق ، الکامل ، کتاب البدایه و النهایه ، اخبار الدول ، المعجم الکبیر طبرانی ، مجمع الزوائد ، کفایه الطالب ، تفسیر قرآن ابن کثیر و مقتل الحسین و همچنین تهذیب التهذیب ابن حجر که اینها همه از منابع مشهور و معتبر اهل سنت هستند .

Katika vyanzo vya Kisunni,tukio hili limeripotiwa kwa upana zaidi hasa katika vyanzo vya Hadithi na Tarekh kama vile:Dhakhairul-Aqba cha Tabari Al-Sha’fiiy,na vile vile katika kitabu cha:Tarekh Dimashqi,Swawa’iqul Muhriqa,Al-Khaswa’isul-Kubra,Yana’biul-Mawadda,Tadhkiratul-Khawa’swi,Siyru Aala’min-Nubala’i cha Dhahbi,Tarekhul-Khulafaa,Kitabu Ihqaqul-Haqqi,Al-Ka’milu,Kitabul-Bida’ya Wan-Niha’ya,Akhbarud-Duwali,Al-Muujamul-Kabir cha Tabrani,Majmauz-Zawa’id,Kifa’yatut-Talib,Tafsirul-Qur’an cha Ibn Kathir na Maqtalul-Husein.Pia Tahdhibut-Tahdhibi cha Ibn Hajar, ambapo vitabu vyote hivyo ni vyanzo mashuhuri vya Kisunni na vyenye itibari kubwa.

و جالبتر اینکه بر خلاف کتاب اروپایی علت بارش این باران از آسمان را نیز بیان نموده اند .

(MSIMULIZI):Na jambo la kuvutia zaidi ni hili kwamba:Katika vitabu hivyo tulivyovitaja –tofauti na vitabu vya Ulaya– kumebainishwa ndani yake sababu iliyopelekea kunyesha kwa Mvua hiyo ya Damu.

در همه کتب و منابع مذاهب اسلامی به اتفاق باران خون را بعد از کشته شدن حسین علیه السلام امام سوم شیعیان و نوه پیامبر اسلام در روز دهم محرم سال ۶۱ هجری قمری عنوان کرده اند که در پی جنگی ناجوان مردانه در سرزمینی به نام کربلا به شهادت رسید و تمام خانواده وی به اسارت گرفته شدند و زینب خواهر یشان در مجلسی خطاب به قاتلین برادرش به این واقعه باران خون اشاره داشته است .

(MSIMULIZI):Katika vyanzo vyote vya Madhehebu ya Kiislam,tukio la Kunyesha Mvua ya Damu, limetajwa kuwa limetokea baada ya kuuliwa Husein (a.s) katika siku ya 10 ya Mwezi wa Muharram,mwaka 61 Hijria,ambaye ni Imam wa Tatu wa Mashia {Wafuasi wa Ahlul-Bait (a.s)},na Mjukuu wa Mtume wa Uislaam (s.a.w.w),ambapo alipata Shahada katika Ardhi iitwayo Karbala,baada ya kuuliwa na Madhalimu katika Ardhi hiyo.Na watu wote wa Familia yake wakafanywa kuwa mateka,na Dada yake Zainab akiwa katika mkusanyiko wa watu,aliwahutubia wauaji wa Kaka yake,na aliashiria katika Tukio hili la Kunyesha kwa Mvua ya Damu.

همینطور وقتی که حضرت زینب سلام الله علیها به دربار یزید رفته بودند و آن خطبه مشهور را ایراد نمودند در اواخر خطبه فرمودند تعجب نکنید اگر بخاطر این مصیبت از آسمان خون ببارد و اگر هر جویبارها پر از خون بشود و اگر چاههای شما در اثر ریزش باران خون پر از خون شود این روایات در کتاب صواعق المحرقه صفحات ۱۱۶ و ۱۹۲ تفسیر ابن کثیر جلد ۹ صفحه ۱۶۲ ذکر شده است.

پس چنین اتفاقی در روز عاشورا در منابع شیعه و اهل سنت متواتر نقل شده است .

Vile vile Hadharat Zainab (s.a) pindi alipoelekea katika Mahakama ya Yazid bin Muawia na kuitoa Hotuba hiyo Mashuhuri,alisema mwishoni wa Hotuba:

Msishangae ikiwa Mbingu itanyesha Mvua ya Damu kwa sababu ya Msiba huu,na ikiwa Mito yote itajaa damu,na ikiwa visima vyenu vitajaa damu kutokana na athari ya Mvua ya Damu”.

Riwaya hii imetajwa ndani ya kitabu kiitwacho: Swawa’iqul-Muhriqa,Ukurasa wa 116,na 192,na Tafsir Ibn Kathir,Mjaladi wa 9,Ukurasa wa 162.

Hivyo tukio hili lililotokea katika Siku ya Ashura,limenukuliwa kwa Tawa’tur ndani ya vyanzo vya Shia na Sunni.

و همچنین در کتاب عیون اخبار رضا از قول امام هشتم شیعیان حضرت رضا علیه السلام اینگونه مینویسد که جدشان امام باقر علیه السلام میفرماید :

(MSIMULIZI):Vile vile Kitabu kiitwacho:Uyuni Akhbarur-Ridha,kutoka katika kauli za Imam wa 8 wa Mashia { Wafuasi wa Ahlul-bait (a.s) },Hadhrat Ridha (a.s),kimenukuu haya yafuatayo kwamba: Babu yake Imam Baqir (a.s) anasema:

لما قتل جدی الحسین امطرت السماء دما و ترابا احمر .

وقتی جدم امام حسین علیه السلام کشته شد که خود حضرت باقر هم درآن واقعه تشریف داشتند و حدود پنج سالشان بود میفرماید وقتی که امام حسین علیه السلام کشته شد آسمان خون و خاک قرمز بارید.

 “Alipouliwa Babu yangu Husein,Mbingu ilinyesha Mvua ya Damu na udongo mwekundu”.

Pindi Babu yangu Husein alipouliwa, ambapo yeye mwenyewe Hadhrat Baqir pia alikuwepo katika tukio la Karbala, na alikuwa na umri takriban wa miaka mitano (5) anasema: Pindi Babu yangu Husein alipouliwa Mbingu ilinyesha Mvua ya Damu na Udongo mwekundu.

به خصوص منابع اهل تسنن این مساله را پذیرفته اند نشان دهنده این است که این مساله حقیقت دارد و اتفاق افتاده حتی کسی مانند زهری که سر سپرده بنی امیه است و کسی مانند ابن عبد ربه آندلسی که در کتاب العقد الفرید به این نکته اشاره میکند که او در آندلس اموی زندگی میکرده و طرفدار بنی امیه بوده است ولی این مسئله را اذعان کرده و به آن اعتراف کرده است .

Hususan vyanzo vya Kisunni,kulikubali Suala hili ni ishara ya wazi inayoonyesha kwamba suala hili lina uhakika na limetokea,hata watu mfano:Zuhri aliyekuwa Mtumishi wa Khilafa ya Bani Umaiiya,na watu wengine kama vile:Ibn Abdi Rabbih Al-Andalus,ambapo katika kitabu chake kiitwacho:Al-Iqdul-Fariydi anaashiria katika nukta hii kwamba:Alikuwa akiishi Andalus ya Banu Umaiyya na alikuwa akiwaunga mkono Bani Umaiyya,lakini hata hivyo alilikubali suala hili,na alilitambua suala hilo.

هر چه به جلو پیش میرویم مطالب جالبتری ما را هدایت میکند از جمله آنکه در منابع تاریخ اسلام این واقعه یعنی بارش خون از سمت پیشوایان و رهبران اسلامی پیشبینی شده و از کیفیت آن حرف به میان آورده اند .

(MSIMULIZI):Kadiri tunavyozidi kusonga mbele,ndivyo tunavyozidi kukutana na maudhui inayovutia zaidi na kutuongoza kama vile ukweli huu kwamba:Vyanzo vya Historia ya Kiislam vimelitabiri tukio hili (yaani tukio la kunyesha Mvua ya Damu) kupitia Maimam na Viongozi wa Kiislaam,na vimezungumzia jinsi na namna lilivyotokea.

در جلد ۴۵ بحار علامه مجلسی بابی را علامه مجلسی آورده در باب گریستن آسمان و اینکه این قرمزی چطور بوده است در جلد ۵۷ باز روایاتی داره در جلد ۷۹ بحار باز روایاتی داره و در کتب روایات شیعه به صورت مفصل این مطلب نقل شده است .

Katika Mjalladi wa 45 wa Biharul-An-waari ya Allamal-Majlisi,tunakuta Allama Majlisi ameweka Mlango Maalum na kuuita:”Mlango wa kulia kwa Mbingu,na kwamba ililia vipi na huu wekundu ulioshuhudiwa ulikuwa namna gani.Na katika Mjalladi wa 57 pia kuna Riwaya kuhusiana na tukio hili.Katika Mjalladi wa 79 wa Biharul-Anwaari pia kuna Riwaya kuhusiana na tukio hili.Na katika vitabu mbalimbali vya Riwaya vya Shia tukio hili limenukuliwa ndani yake na kuelezwa kwa ufafanuzi zaidi.

در ادامه کنکاشمان به روایاتی در همین خصوص یعنی پیشبینی بارش خون برخوردیم :

ام سلمه یعنی همسر پیامبر اسلام پیش بینی امام سوم شیعیان در سرزمین کربلا و وقوع این اتفاق را از قول رسول خدا نقل کرده است که این مطلب در کتب المجمع الکبیر ، مجمع الزوائد و کنز العمال مستند میباشد .

(MSIMULIZI):Tukiendelea na jitihada yetu (katika kutafuta uhakika na ukweli) tumekutana na Riwaya kuhusiana na maudhui hii yaani utabiri wa Kunyesha Mvua ya Damu kama ifuatavyo:

Ummua Salama,yaani Mke wa Mtume wa Uislaam (s.a.w.w),amenukuu Kauli ya Mtume (s.a.w.w) ikitabiri tukio linalohusiana na Imam wa tatu (3) wa Mashia  katika Ardhi ya Karbala, ambapo maudhui hii imenukuliwa ndani ya vitabu hivi viitwavyo:Majmaul-Kabir ,Majmauz-Zawa’idi na Kanzul-Umma’li.

در حدیثی از میثم تمار سلام الله علیه از حضرت امیر المومنین علیه السلام اینچنین نقل شده که وقتی حضرت خبر شهادت فرزندشان حسین را دادند فرمودند که در شهادت او همه چیز گریه میکند : و تمطر السماء دما و رمادا ، و آنگاه است که آسمان خون و خاکستر خواهد بارید .

Imenukuliwa katika Hadithi kutoka kwa Maithamu Tamma’ru (Amani iwe juu yake),kutoka kwa Hadhrat Amirul-Muuminina (a.s) kwamba:Pindi Hadhrat Amirul-Muuminina (a.s) alipozitoa habari za kuuliwa kwa Mwanae Husein (a.s) alisema kwamba: Katika Shahada yake kila kitu kitalia:

“و تَمطِرُ السَّماءُ دَماً و رِماداً”

Kisha Mbingu itanyesha Mvua ya Damu na Majivu.

و همچنین شیخ صدوق از علماء شیعه در کتاب خود ,به نام امالی ذکر کرده است که امام دوم شیعیان حسن علیه السلام در لحظات پایانی خود خطاب به برادرشان حسین علیه السلام گفتند : هیچ روزی روز شهادت تو نمیشود و روزی که از آسمان خون میبارد و این پیش بینی سالها قبل از وقوع بوده .

(MSIMULIZI):Vile vile  Sheikh Swaduq ambaye ni miongoni mwa Maulamaa wa Kishia,ametaja ndani ya kitabu chake kiitwacho A’ma’li kwamba:Imam wa pili wa Mashia  Hasan (a.s),alisema katika dakika ya mwisho ya maisha yake kumwambia kaka yake Husein (a.s):

Hakuna siku itakayolingana na siku ya Shahada yako,na siku ambayo Mbingu itanyesha Mvua ya Damu”.

Na utabiri wa namna hii ulitolewa kabla ya tukio hilo kwa miaka kadhaa.

حال بعد از گذاردن گوشه های تحقیق و کنکاش مان کنار هم به چند نکته قابل توجه دست مییابیم .

با رجوع به کتابهای تاریخ اروپا دست یافتیم که در سالهای ۶۸۴ و ۶۸۵ میلادی سالهایی هستند که بارش خون در آن ذکر شده در حالی که واقعه عاشورا در سال ۶۸۰ میلادی بوده است .

به راستی این تفاوت سال را چگونه میتوانیم توجیه کنیم ؟

پاسخ بسیار ساده است طبق گفته پروفسور ریچارد نورس نگارش این کتب تاریخ اروپایی به سیصد سال بعد از وقوع عاشورا بر میگردد پس مبنای این نوشته ها تاریخ شفاهی بوده است . بنابر این احتمال خطای چهار یا ۵ سال امری طبیعی خواهد بود و این در حالی است که در منابع تاریخی اسلام وقوع تاریخ باران خون همگی در یک تاریخ عنوان شده است .

و همچنین مبنای تاریخ میلادی گذشت روزها است اما طلوع ماه و شبها مبنای تاریخ قمری است و خود این تفاوت مبنی میتواند ایجاد کمی اختلاف در شماره آن باشد .

و اما باران خونی که در تاریخ اروپا و کتب اسلامی از آن یاد شده آیا واقعا خون بوده و یا تنها رنگش قرمز رنگ بوده است.

(MSIMULIZI):Hivyo baada ya kuelekea na kutoka katika pembe za utafiti na jitihada zetu,ungana nasi kwa pamoja katika nukta hizi kadhaa na muhimu tulizoweza kuzifikia:

Baada ya kurejea katika Vitabu vya Kihistoria vya Ulaya,tumekuta kwamba:Mwaka 684 A.D na mwaka 685 A.D ni miaka iliyotajwa ndani yake tukio la kunyesha kwa Mvua ya Damu,ambapo kutokea kwa tukio la A’shura ilikuwa ni mwaka 680 A.D.

Swali la kujiuliza:Tunawezaje kuitafsiri tofauti hii inayojidhihirisha?.

Jibu la swali hili ni rahisi mno, kwa mujibu wa kauli ya Richard Nursi:Uandikwaji wa vitabu hivi vya Kihistoria vya Ulaya ilikuwa ni baada ya miaka mia moja (100) tangu kutokea kwa tukio la Ashura,Hivyo msingi wa Historia hiyo katika vitabu hivyo vya Ulaya ulikuwa ni Masimulizi.Kwa mantiki hiyo ihtimali ya kukosea miaka minne (4) au mitano (5) litakuwa ni jambo la kawaida,na ukizingatia kwamba vyanzo vyote vya Historia ya Kiislaam,vimelitaja Tukio hilo la Kihistoria la kunyesha kwa Mvua ya Damu katika tarehe moja bila ya kuhitilafiana.

Vile vile msingi wa Tarehe za Miladia (A.D) ulikuwa ni kuhesabu Mchana,ama kuchomoza kwa Mwezi na Usiku ilikuwa ni msingi wa Tarehe za Qamari,na tofauti ya msingi kama hii inaweza kuleta tofauti kidogo katika kuhesabu mwaka wa kutokea kwa tukio hilo.

*Ama Mvua ya Damu,iliyotajwa katika Vitabu vya Kihistoria vya Ulaya na Vitabu vya Kiislaam,je, ni kweli kabisa ilikuwa ni Mvua ya Damu au rangi yake ilikuwa ni rangi Nyekundu tu na haikuwa damu halisi?.

تفاوت بسیار مهمی بین باران خونی که در این کتابها شرح داده شده و اتفاقی که در جاهای دیگر مانند کرلای هند که بارانی به رنگ قرمز گزارش شده و حقیقتا گل قرمز بوده وجود دارد.

اما فرق بین اتفاقی که در کتب اروپایی و جهان اسلام ذکر شده و باران قرمز هند این است که کسانی که این وقایع را ثبت کرده اند دانشمند بودند و این موضوع را دقیقا خون گزارش کرده اند و نه چیزی شبیه به خون و در بسیاری از موارد جنس و لختگی خونی که از آسمان باریده بود صحبت کردند و مخصوصا کلمه خون تازه را بکار برده اند و ما را به این نتیجه میرساند چیزی که آنها گزارش میکنند به دید آنها واقعا خون بوده و نه چیزی شبیه به خون .

Ni tofauti muhimu sana kati ya Mvua ya Damu iliyoelezwa katika vitabu, na tukio lingine lililoripotiwa katika maeneo mengine kama vile:Karla nchini India,ambapo kulilipotiwa tukio la kunyesha kwa Mvua ya rangi nyekundu,na hakika udongo mkubwa ulionekana katika Mvua au ndani ya Maji.

Ama tofauti iliyopo kati ya tukio lililotajwa ndani ya Vitabu vya Ulaya na Ulimwengu wa Kiislam, na lile tukio la kunyesha Mvua ya rangi nyekundu nchini India ni hii kwamba:Watu walio thibitisha matukio haya walikuwa ni Maulamaa (na Wanazuoni),na hakika waliripoti tukio hili kuwa ni tukio la damu halisi na sio tu kitu kinachofanana na damu,na walizungumzia katika sehemu kadhaa kuhusiana na aina ya mchanganyiko wa damu iliyonyesha toka Mbinguni,hasa ukizingatia kwamba wametumia neno DAMU katika ibara zao.Hivyo wanatufikisha katika natija hii kwamba:Kitu wanachokiripoti kwa muono wao ilikuwa ni damu halisi na sio kitu kinachofanana na damu.

صواعق الحرقه از ابی سعید نقل میکند : و آسمان نیز خون میبارید و اثرش تا مدتها در لباسها باقی بود تا اینکه این لباسها پاره پاره شد . یعنی این خونها پاک نمیشد هر چه میشستیم و اثر آن باقی بود تا لباسها پاره شود .

Imenukuliwa ndani ya Swawa’iqul-Muhriqa kutoka kwa Abi Said kwamba amesema:

Pia na Mbingu ilikuwa ikinyesha Mvua ya Damu, na athari ya damu ilikuwa inabaki kwa muda mrefu juu ya nguo, kiasi kwamba mpaka nguo zichanike chanike ndio athari ya damu inatoweka.Kwa maana kwamba Damu hiyo ilikuwa haitoweki kwenye nguo, kila tulipokuwa tukijaribu kufua nguo,basi athari yake ilikuwa inabaki mpaka nguo zitakapochanika chanika.

و شاید این نکته نیز قابل توجه باشد که بارش خون  به علت کشته شدن حسین علیه السلام در کتب تاریخ اروپا ذکر نشده است .

چرا ؟

 (MSIMULIZI):Na pengine huenda nukta hii ikawa ni nukta muhimu ya kuzingatia kwamba tukio la kunyesha Mvua ya Damu haikutajwa ndani ya vitabu vya Ulaya kuwa sababu yake ilikuwa ni kuuliwa kwa Imam Husein (a.s).

Kwa nini?!.

در اروپای غربی بعد از فروپاشی روم غربی مناطقی که از ایتالیا به طرف غرب اروپا هست دچار یک از هم گسیختگی و حکومتهای محلی مستقل و معارض نسبت به همدیگر شد و چراغ علم و تمدن در اینها خاموش شد لذا به یک جهالت قهقری رفتند اروپا در آن موقع در عقب ماندگی علمی به سر میبرد و انگلستان هم جزئی از این اروپا بود که اتفاقا اهمیتش نسبت به بقیه اروپا به دلیل جزیره بودن کمتر بود .  

Katika upande wa Ulaya Magharibi baada ya kuanguka kwa Roma Magharibi sehemu za Italia zilizopo upande wa Magharibi mwa Ulaya zilizokuwa zimeungana ziligawanyika, na zikaundwa Serikali za mitaa zinazojitegemea na zikawa na migogoro na uadui zenyewe kwa zenyewe kiasi kwamba mpaka ile Taa ya Elimu na Ustaarabu ikazimika katika serikali hizo.Hivyo walirudi kinyume nyume katika ujinga.Ulaya kwa wakati huo ilizidi kurudi (na kubaki) nyuma katika elimu,na Uingereza pia ilikuwa ni eneo moja wapo la  Ulaya na umuhimu wake ulikuwa ni mdogo sana  ukiilinganisha na maeneo mengine ya Ulaya, na hii ni kutokana na kwamba Uingereza ni Kisiwa.

از صحبتهای کارشناس مربوطه چنین برداشت میشود که در زمان نوشتن تاریخ اروپایی به دلیل عدم تمدن اصلی امکان ثبت دقیق و علمی وقایع وجود نداشته است حال چه برسد به دلیل این وقایع .

(MSIMULIZI):Mazungumzo ya wataalam yanahusiana na fikra kama hii ambapo katika zama za uandikwaji wa Historia ya Ulaya, haukuwepo uwezekano wa kusajili kumbukumbu sahihi za matukio ya kielimu.Hivyo inakuwa ni vigumu katika hali kama hiyo kuifikia dalili ya matukio kama hayo.

و حالا  در پایان بعد از اینهمه تحقیق و جستجو که منجر به ساخت این مستند گردیده به این نقطه رسیدیم که تنها یک روز فقط یک روز از شرق گرفته تا غرب باران خون باریده است و آن روز به شهادت رسیدن مظلومانه حسین ابن علی علیه السلام بوده که به گفته تمامی اشخاص و افکار و تمامی ادیان جهان ایشان یکی از تاثیر گذار ترین افراد طول تاریخ بشری بوده است.

(MSIMULIZI): Hivyo, baada ya tahkiki na utafiti wote huo ambao ni sababu ya kutengeneza Filamu hii ya Documentary, tumeweza kufikia nukta hii ifuatayo kwamba:

Mvua ya Damu ilinyesha kwa siku moja, siku moja tu kuanzia pande za Mashariki hadi Magharibi, na siku hiyo ilikuwa ni siku ya Shahada ya Madhulumu Husein bin Ali (a.s),ambapo kutokana na kauli za watu wote,na fikra za watu wote, pamoja na dini zote za Ulimwengu mzima,inadhihirika wazi kwamba Husein (a.s) alikuwa ni miongoni mwa watu wenye ushawishi mkubwa zaidi katika Historia ya Mwanadamu.

سلام آقای دکتر بالرام  شکلا

سلام من باران شکلا هستم

ببخشید درست است که شما هندو مذهی هستید ؟

بله ، من هندو هستم .

میخواستم نظر شما را در مورد شخصیت امام حسین بدانم ؟

ببینید امام حسین در هندوستان و بین هندوها خیلی با عظمت میباشد ، بخاطر اینکه ایشان شهید شدند در راه حق تعالی و بخاطر ما،و فکر میکنیم که حسین علیه السلام بخاطر این انسانیت برای همه میتوانند رهبر بشوند .

سوال دارم:آیا اینقدر شخصیت امام حسین علیه السلام مهم است که بخاطر شهادت ایشان از آسمان خون ببارد.وقتی که مردان خدا ظلم و تظلم میبینند همه کائنات گریه میکنند در این هیچ شکی نیست و همه کائنات خون گریه میکنند.

 

Salam Dakta Bolam  Shokla.

Salam,mimi ni Bolam Shokla.

Sahamani,ni kweli kwamba wewe ni mtu wa Madhehebu ya Hindu?.

Ndio,mimi ni Hindu.

Nilitaka kujua maoni yako kuhusiana na Shakhsia ya Imam Husein (a.s)?.

Tizama,Imam Husein (a.s) alikuwa na adhama kubwa sana nchini India na baina ya Wahindi,na hii ni kwa sababu yeye aliuliwa Shahidi katika njia ya Mwenyeezi Mungu (s.w) na kwa  ajili yetu,na tunafikiri kwamba Husein (a.s) kwa sababu ya utu na ubinadamu kama huu,anaweza kuwa kiongozi wa watu wote.

Swali la pili:Je,ni kweli kwamba Shakhsia ya Imam Husein (a.s) ni muhimu kiasi hicho, kiasi kwamba mpaka Mvua ya Damu inyeshe kwa sababu ya Shahada yake ?.

Pindi watu wa Mwenyeezi Mungu (s.w) wanapokumbana na dhulma na ukandamizaji,basi viumbe vyote hulia na kububujikwa na machozi,na hakuna shaka yoyote kuhusiana na hilo,hivyo viumbe vyote vinatoa machozi kumlilia Husein (a.s).

IMETARJUMIWA NA KUWEKWA KATIKA LUGHA YA KISWAHILI NA: SHEIKH TAQEE ZACHALIA

ارسال یک پاسخ

Barua pepe yako haitachapishwa.
Sehemu ya lazima imeonyeshwa kwa alama ya * .

*


Wasiliana nasi | RSS | Ramani ya Tovuti

Haki zote za Tovuti hii Islam 14 zimehifadhiwa,hivyo inaruhusiwa kutumia makala yoyote ya tovuti hii sambamba na kutaja chanzo chake.