Makala mpya

Dhamini kazi yetu

Gazeti: Saudia itazidi kutengwa kwani imejitakia

11Utawala wa Saudi Arabia utazidi kutengwa na mataifa mengi duniani kutokana na hatua yake ya kumuua shahidi mwanazuoni maarufu wa Kiislamu, hatua zake dhidi ya Iran na vitendo vingine vingi dhidi ya ubinadamu vya watawala wa Riyadh.
Kwa mujibu wa tahariri ya leo ya gazeti la Jomhuri Islami linalochapishwa hapa Tehran, uzoefu unaonyesha kuwa mahesabu na mbinu zinazotumiwa na utawala wa Saudia hufeli. Watawala wa Saudia wanaibua migogoro na machafuko katika eneo huku wakivuruga hali ya mambo ndani ya nchi hiyo na kuharibu uhusiano na majirani pamoja na ulimwengu wa Kiislamu; sera ambazo haziwezi kuwa na maslahi na wao.
Mhariri wa gazeti la Jomhuri Islami ameendelea kuandika kuwa hata vyombo vya habari vya nchi ambazo ni waitifaki wa Saudia vimelalamikia wazi kuuawa Sheikh Nimr Baqir al Nimr, msomi maarufu wa Kiislamu na mwanamapambano dhidi ya ubaguzi, dhulma na ukosefu wa uadilifu.
Mhariri huyo ameandika kuwa kwa miaka mingi sasa watawala wa Saudi Arabia wamekuwa wakiibua migogoro ndani na nje ya ufalme huo.

ارسال یک پاسخ

Barua pepe yako haitachapishwa.
Sehemu ya lazima imeonyeshwa kwa alama ya * .

*


Wasiliana nasi | RSS | Ramani ya Tovuti

Haki zote za Tovuti hii Islam 14 zimehifadhiwa,hivyo inaruhusiwa kutumia makala yoyote ya tovuti hii sambamba na kutaja chanzo chake.