Makala mpya

Dhamini kazi yetu

Mtazamo wa Kiongozi Muadhamu kuhusu utekelezaji wa mpango wa JCPOA na malengo ya Marekani

tvshia-304Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema kuwa mafanikio yaliyopatikana katika uga wa nyuklia ni matunda ya jitihada na utaalamu wa wasomi wa Iran wakiwemo mashahidi wa nyuklia na uungaji mkono wa kila hali wa taifa la Iran kwa suala hilo. Vile vile amesema kujitokeza kwa wingi wananchi wa Iran katika uchaguzi wa tarehe 26 Februari hapa nchini kutadumisha amani na heshima ya taifa la Iran na kutadhamini ustawi na maendeleo ya Jamhuri ya Kiislamu.
Ayatullah Ali Khamenei amesema hayo leo mbele ya maafisa wanaosimamia zoezi la uchaguzi wa awamu ya 10 ya Bunge la Iran na awamu ya tano ya Baraza la Wataalamu wanaomchagua na kusimamia kazi za Kiongozi Muadhamu. Vile vile ameashiria kuanza kutekelezwa makubaliano ya nyuklia kupitia mpango wa JCPOA na kubainisha kuwa, pande zilizofanya mazungumzo na Iran zilikuwa zinajua vyema kuwa Tehran haina nia ya kumiliki bomu la nyuklia na ndio maana tunasema, zilikuwa na malengo yao mengine kabisa. Utekelezaji wa makubaliano ya nyuklia kati ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na kundi la 5+1 ulianza rasmi usiku wa Jumamosi tarehe 16 Januari 2016. Kumalizika suala hili la kupandikiza kumethibitisha rasmi usahihi wa sisitizo la Iran kuwa miradi yake ya nyuklia haijawahi kuwa na malengo ya kijeshi kama ambavyo kumezidi kuonesha uongo wa madai ya maadui wa Iran kuhusu suala hilo. Kama alivyosema Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu, tangu mwanzo kabisa, nchi zote hizo zilikuwa zinajua vyema kuwa miradi ya nyuklia ya Iran ni ya amani na si ya kijeshi lakini zilitumia suala hilo kama kisingizio cha kutaka kuudhofisha mfumo wa Jamhuri ya Kiislamu na kujaribu kuushinda nguvu muqawama wa taifa la Iran, hata hivyo lakini wameshindwa. Amesema, lengo kuu la kambi ya kibeberu katika kushadidisha mashinikizo kwenye suala la nyuklia, ni kujaribu kukwamisha harakati kuu – inayozidi kupiga hatua za maendeleo – ya taifa la Iran na kujaribu kukabiliana na ushawishi unaozidi kuongezeka kila leo wa Jamhuri ya Kiislamu katika eneo hili na duniani kiujumla. Lengo la mabeberu la kutaka kufanikisha njama zao hizo, lilikuwa ni kujaribu kuyaonesha mataifa mengine duniani kuwa, Jamhuri ya Kiislamu nayo imeshindwa kuunda na kuudumisha mfumo wa utawala uliosimama juu ya misingi ya kidini. Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ameeleza masuala muhimu yanayohusiana na utekelezaji wa makubaliano ya nyuklia kati ya Iran na kundi la 5+1 na kuwaambia maafisa wa serikali kwamba: Marekani ndiyo ile ile Marekani ya zamani, kwa msingi huo kuna ulazima wa kuwa macho mbele ya hadaa zake katika utekelezaji wa makubaliano hayo. Ayatullah Khamenei amesema kwa kuzingatia kuwa matunda ya nyuklia ni matokeo ya juhudi na umahiri wa wasomi wa Iran na uungaji mkono wa taifa; si insafu kwa baadhi ya watu kueneza propaganda kuwa matunda haya ni matokeo ya fadhila za Marekani! Aidha amesisitizia wajibu wa kuwa macho mbele ya njama za Marekani na kusema kuwa, lengo kuu la Marekani ni kutumia mabavu na propaganda kufikia malengo yake, hivyo watu wote wanapaswa kuwa macho na wasimame kidete kukabiliana na njama hizo. Amesema iwapo Marekani itakwepa kutekeleza ahadi zake kuhusu mpango wa JCPOA, inabidi Iran nayo ifanye vivyo hivyo kwa kiwango itakachofanya Marekani. Akiashiria sifa nyingine ya Marekani, Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema: Matukio ya sasa katika eneo la Mashariki ya Kati yameweka wazi malengo na makusudi ya miaka kadhaa iliyopita ya Wamarekani ya udharura wa kuanzishwa Mashariki ya Kati mpya; kwani Mashariki ya Kati mpya ya Wamarekani ni Mashariki ya Kati yenye vita, ugaidi, chuki na taasubi na iliyojaa mapigano ya kimadhehebu na ya ndani. kwa kweli mapigano yanayoongezeka kila leo katika eneo la Mashariki ya Kati na kaskazini mwa Afrika asili yake ni njama za Marekani na kujiingiza waskari wa nchi hiyo katika masuala ya kisiasa na kijeshi ya eneo hili. Kwa kuzingatia yote hayo, ndipo linapozuka swali hapa, vipi mtu anaweza kuiamini Marekani kwa kudai tu inapigania demokrasia na amani wakati sifa ya Marekani ni kueneza machafuko kwa ajili ya kufanikisha malengo yake ya kibeberu? Ni kwa sababu hiyo hiyo ndio maana Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu akasisitiza kuwa, Marekani itabakia kuwa ni Marekani ile ile hata baada ya kumalizika kadhia ya nyuklia na kuanza kutekelezwa makubaliano kati ya Iran na kundi la 5+1.

ارسال یک پاسخ

Barua pepe yako haitachapishwa.
Sehemu ya lazima imeonyeshwa kwa alama ya * .

*


Wasiliana nasi | RSS | Ramani ya Tovuti

Haki zote za Tovuti hii Islam 14 zimehifadhiwa,hivyo inaruhusiwa kutumia makala yoyote ya tovuti hii sambamba na kutaja chanzo chake.