Makala mpya

Dhamini kazi yetu

NI IPI HIJABU YA KISHERIA ILIYOKAMILIKA?

83594-250353-1405334562Hijabu (Stara) ya kisheria ziko aina mbili: Ya dhahiri na dhati.

Ama hijabu ya dhahiri: ni ile hijabu ambayo Mwenyezi Mungu amewaamuru wasichana na wanawake kujihimiza kufuatilia wasifa wake, kama vile kusitiri miili yao mbele ya wanaume ajinabi na wasio waume zao, ameamrisha hilo katika Qur’ani tukufu, na kuthibitishwa na maneno ya Mtume Mtukufu (s.a.w.w) na Maimamu masumiin (a.s).

Aidha maulamaa wa fiqhi wamepambanua Zaidi suala hilo, na sisi twaliashiria kwa muhtasari.

Wajibu wa kuvaa hijabu ni; Msichana au mwanamke kusitiri viungo vyake kiukamilifu, ila isipokuwa uso na mikono yake kwa wasiokuwa waume zao na ajinabi, na si maalumu kwa juba pekee ila vazi linalositiri mwili kamili kwa wengine na kutotamanisha maumbile yake.

  • Naama yampasa atakaye kujistiri kuzingatia wasifa zifuatazo:
  1. Asiwe anavutia.
  2. Asiwe amevaa mavazi yanayombana (yanachonga mwili) kiasi kwamba hudhihirisha viungo vya mwili wake.
  3. Asivae mavazi mepesi (yatakayoonesha viungo ambavyo ni wajibu kuvistiri).

Kama mambo hayo yalizotajwa yatakutana katika hii stara basi itakuwa ni stara ya kisheria, hata kama katika sehemu ya mvaaji wa stara hiyo itakuwa (vazi la) tisheti na suruali iliyo pana. Na hapa ni muhimu kukumbusha ya kuwa pia kufunika miguu ni wajibu kwa ajinabi, na hakuna tofauti kustiri kwa soksi au vinginevyo.

  • Ni wazi kwamba; ikiwa hijabu itakuwa ni ya heshima itakuwa ni bora zaidi kuliko ya fedheha.

Ama hijabu ya dhati: Ni ile ambayo Mwenyezi Mungu amemuamuru Msichana na Mwanamke kama alivyowaamuru Vijana na wanaume katika Qur’ani tukufu, na kuthibitishwa na maneno ya Mtume Muhammad (s.a.w.w) na Maimamu masumiin (a.s).

Na madhumuni ya hijabu (stara) ya dhati ni; Ile mwanadamu kujizuia na machafu ya ufisadi na kila kitakacho mghadhibisha Mwenyezi Mungu mtukufu, kwa maana kwamba; Uchamungu, kujiheshimu na kufumba macho kuangalia ya haramu, pia hijabu ya dhati ni ile; Inayohusu mienendo ya Msichana na Mwanamke, aidha Mvulana na Mwanamume, ambayo ni muhimu mno, ambapo hijabu (stara zote mbili) hukamilika pindi iwapo nyingine, hivyo hakuna maana ya stara ila kwa kulinda taratibu zake.

Anasema Mwenyezi Mungu:

﴿… وَإِذَا سَأَلْتُمُوهُنَّ مَتَاعًا فَاسْأَلُوهُنَّ مِن وَرَاء حِجَابٍ ذَلِكُمْ أَطْهَرُ لِقُلُوبِكُمْ وَقُلُوبِهِنَّ… ﴾.

“…Na mnapo wauliza wakeze haja waulizeni nyuma ya mapazia. Hivyo ndio usafi zaidi kwa nyoyo zenu na nyoyo zao…” Ahzaab; 53.

﴿قُل لِّلْمُؤْمِنِينَ يَغُضُّوا مِنْ أَبْصَارِهِمْ وَيَحْفَظُوا فُرُوجَهُمْ ذَلِكَ أَزْكَى لَهُمْ إِنَّ اللَّهَ خَبِيرٌ بِمَا يَصْنَعُونَ * وَقُل لِّلْمُؤْمِنَاتِ يَغْضُضْنَ مِنْ أَبْصَارِهِنَّ وَيَحْفَظْنَ فُرُوجَهُنَّ وَلَا يُبْدِينَ زِينَتَهُنَّ إِلَّا مَا ظَهَرَ مِنْهَا وَلْيَضْرِبْنَ بِخُمُرِهِنَّ عَلَى جُيُوبِهِنَّ وَلَا يُبْدِينَ زِينَتَهُنَّ إِلَّا لِبُعُولَتِهِنَّ أَوْ آبَائِهِنَّ أَوْ آبَاء بُعُولَتِهِنَّ أَوْ أَبْنَائِهِنَّ أَوْ أَبْنَاء بُعُولَتِهِنَّ أَوْ إِخْوَانِهِنَّ أَوْ بَنِي إِخْوَانِهِنَّ أَوْ بَنِي أَخَوَاتِهِنَّ أَوْ نِسَائِهِنَّ أَوْ مَا مَلَكَتْ أَيْمَانُهُنَّ أَوِ التَّابِعِينَ غَيْرِ أُوْلِي الْإِرْبَةِ مِنَ الرِّجَالِ أَوِ الطِّفْلِ الَّذِينَ لَمْ يَظْهَرُوا عَلَى عَوْرَاتِ النِّسَاء وَلَا يَضْرِبْنَ بِأَرْجُلِهِنَّ لِيُعْلَمَ مَا يُخْفِينَ مِن زِينَتِهِنَّ وَتُوبُوا إِلَى اللَّهِ جَمِيعًا أَيُّهَا الْمُؤْمِنُونَ لَعَلَّكُمْ تُفْلِحُونَ﴾.

“Waambie Waumini wanaume wainamishe macho yao, na wazilinde tupu zao. Hili ni takaso bora kwao. Hakika Mwenyezi Mungu anazo khabari za wanayo yafanya. Na waambie Waumini wanawake wainamishe macho yao, na wazilinde tupu zao, wala wasionyeshe uzuri wao isipo kuwa unao dhihirika. Na waangushe shungi zao juu ya vifua vyao, wala wasionyeshe uzuri wao ila kwa waume zao, au baba zao, au baba wa waume zao, au watoto wao, au watoto wa waume zao, au kaka zao, au wana wa kaka zao, au wana wa dada zao, au wanawake wenzao, au iliyo wamiliki mikono yao ya kuume, au wafwasi wanaume wasio na matamanio, au watoto ambao hawajajua mambo yaliyo khusu uke. Wala wasipige chini miguu yao ili yajuulikane mapambo waliyo yaficha. Na tubuni nyote kwa Mwenyezi Mungu, enyi Waumini, ili mpate kufanikiwa”. An-nur, 30-31.

﴿يَا أَيُّهَا النَّبِيُّ قُل لِّأَزْوَاجِكَ وَبَنَاتِكَ وَنِسَاء الْمُؤْمِنِينَ يُدْنِينَ عَلَيْهِنَّ مِن جَلَابِيبِهِنَّ ذَلِكَ أَدْنَى أَن يُعْرَفْنَ فَلَا يُؤْذَيْنَ وَكَانَ اللَّهُ غَفُورًا رَّحِيمًا﴾.

“Ewe Nabii! Waambie wake zako, na binti zako, na wake za Waumini wajiteremshie nguo zao. Hivyo ni karibu zaidi kuweza kutambulikana wasiudhiwe. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusamehe, Mwenye kurehemu”. Ahzaab; 59.

و في الختام نبتهل الى الله و نقول: اللهم ارزقنا توفيق الطاعة و بُعدَ المعصية و صدق النية و عرفان الحرمة .

Mwishoe tumuelekee Mwenyezi Mungu kwa muomba:

“O’ Allah! Turuzuku taufiki ya kukutii wewe na tuepushie maasi na nia njema na maarifa ya juu ya kutambua uliyoharamisha.

و اغضض ابصارنا عن الفجور و الخيانة

Zuia macho yetu na maovu na hiana.

و تفضَّل على الشباب بالانابة و التوبة

 Wajaalie vijana muelekeo bora na toba sahihi.

و على النساء بالحياء و العفة .

Na jaalia wanawake haya na uchamungu”.

Imeandaliwa na:

Juma R. Kazingati

ارسال یک پاسخ

Barua pepe yako haitachapishwa.
Sehemu ya lazima imeonyeshwa kwa alama ya * .

*


Wasiliana nasi | RSS | Ramani ya Tovuti

Haki zote za Tovuti hii Islam 14 zimehifadhiwa,hivyo inaruhusiwa kutumia makala yoyote ya tovuti hii sambamba na kutaja chanzo chake.