Makala mpya

Dhamini kazi yetu

NI AKINA NANI WALIOLAANIWA?

devil

Kutoka kwa Yunus bin Yaaqub, amesema; Nilimsikia Saadiq Jaafar bin Muhammad (as) akisema katika hadithi: “Ee Yunus:

 1. Amelaaniwa amelaaniwa atakaemuudhi Jirani yake.
 2. Amelaaniwa amelaaniwa Mwanamume atakaeanziwa na ndugue kuomba suluhu na asikubali suluhu yake.
 3. Amelaaniwa amelaaniwa mbeba Qur’ani na ilihali anang’ang’ania kunywa Pombe.
 4. Amelaaniwa amelaaniwa Mwanachuoni anaemtawalisha Sultan jeuri akimsaidia katika kutenda shari.
 5. Amelaaniwa amelaaniwa amchukiaye Ali bin Abitalib (as), kwani hakumchukia ila amemchukiza Mtume wa Mungu (s.a.w.w), na atakaemchukiza Mjumbe wa Mungu (s.a.w.w) basi Allah atamlaani Duniani na Akhera pia.
 6. Amelaaniwa amelaaniwa atakaye mtuhumu Muumini kwa ukafiri, na atakaye mtuhumu Muumini kwa ukafiri ni kama amemuua.
 7. Amelaaniwa amelaaniwa Mwanamke anayemuudhi Mumewe na kumbughudhi. Wema ulioje! Wa mwanamke anayemkirimu mumewe na kutomuudhi, na Wema ulioje! Wa mwanamke atakaye mtii katika kila hali –akaendelea kusema-
 8. Amelaaniwa amelaaniwa anaevunja undugu.
 9. Amelaaniwa amelaaniwa atengenezae urafiki kwa uchawi.
 10. Amelaaniwa amelaaniwa atakaesema: Imani ni maneno na si amali.
 11. Amelaaniwa amelaaniwa atakayeruzukiwa Mali na Mwenyezi Mungu kisha asitoe chochote (katika mali ile) sadaka, je! Hukumsikia Mtume (s.a.w.w) akisema: Sadaka ya dirham moja ni bora zaidi kuliko Sala ya mausiku ishirini.
 12. Amelaaniwa amelaaniwa atakaye mpiga Baba yake au Mama yake.
 13. Amelaaniwa amelaaniwa atakaye dharau Wazazi wake wawili.
 14. Amelaaniwa amelaaniwa asiyeheshimu Msikiti.

Na: Juma R. Kazingati.

ارسال یک پاسخ

Barua pepe yako haitachapishwa.
Sehemu ya lazima imeonyeshwa kwa alama ya * .

*


Wasiliana nasi | RSS | Ramani ya Tovuti

Haki zote za Tovuti hii Islam 14 zimehifadhiwa,hivyo inaruhusiwa kutumia makala yoyote ya tovuti hii sambamba na kutaja chanzo chake.