Makala mpya

Dhamini kazi yetu

Welayatul faqiih

155_64604

Wilayatul Faqiih ni katika mas’ala ambayo yalikitumika katika milango mbalimbali ya Fiqh za kishia. Ama zipo dalili zilizopelekea Wilayatul Faqiih kuzungumziwa kwa uchache, ni kwa sababu:

 1. Suala hili kwa ukosefu wa mazingira ya kulitumia na kulifanyia kazi, ambapo pia ilikuwa ni; Kwa sababu ya Uongozi dhalimu na watawala waovu.
 2. Ilielezewa katika milango tofauti tofauti ya Fiqh, na haukua katika Mlango wenye kujitegemea kama ilivyo kwa sasa.
 3. Wilayatul Faqiih ilitambulika kwa anuani zifuatazo: mfano: Hakimu, Sultani wa Kiislamu, Naibu wa Imamu, Mwenye kusimamia mambo ya Waislam (Aliyeteuliwa na Imam)…
 • Nukta nyingine juu ya Wilayatul Faqiih ni hizi zifuatazo:
 1. Nini maana ya Wilayatul Faqeeh?

@@ Katika Lugha ya kiarabu neno: (وليّ) lina maana ya: Rafiki, Jamaa, na Msaidizi.

(الولاية): Usultani na Cheo. Uongozi na serikali.

@@ Istilahi ya neno hilo kwa mujibu wa elimu ya Fiqh ni kwamba:

 1. Walii ima ni; Yule asiyeweza kujiongoza mwenyewe, huyo atahitaji kuongozwa, mfano ni: Maiti. Mwendawazimu. Majinuni na Mtoto mdogo.
 2. Na walii ni; Yule anaweza kujiongozea mambo yake mwenyewe, na kuweza kuongoza wengine.
 3. Majukumu ya Mwanasheria wa Fiqh ni yepi?

Kutoa fatua za kisheria. Kuhukumu. Na kuongoza serikali.

 1. maJukumu ya Utawala wake ni yepi?
 • Kusimamia mali za asiyekuwepo.
 • Kusimamia suala la kuchukua Khumsi na Zakat na Waqf zote.
 • Kusimamia suala la kutekeleza Adhabu za Kisheria.
 • Kusimamia suala la kuamrisha mema na kukemea mabaya.
 • Kusimamia suala la kuongoza serikali kama: Kupangilia nidhamu za Miji. Kulinda mipaka ya Nchi. Kuzuia kile ambacho kitapelekea kuharibu nidhamu na mpangilio mzima wa jamii ya Waislamu na masilahi ya wote.
 1. Dalili za kuwepo Mtawala wa kisheria?
 2. Dalili ya kiakili:

Ni wazi kwamba jamii inahitajia kiongozi na muendesha mambo ya Waislamu yatakayokuwa yamefungamana na Mambo yote ya kidini yasiyotoka kwenye wigo wa Dini ya Kiislamu.

Hivyo iwapo serikali itaongoza kwa mujibu wa hukumu na sheria zitakazo mridhisha Mwenyezi Mungu na kufuata misingi ya Dini, basi Akili inahukumu kuwa ni lazima awepo Mtu atakaye ongoza serikali hiyo, atakaye kuwa mjuzi wa sheria za Mungu na kusimamia Nyadhifa zake ipasavyo. Hivyo basi iwapo Maasumi atakuwa hadhiri katika jamii hiyo, basi hatuna budi kukubali kuwa Yeye ndiye anaye stahiki Cheo hicho. Na asipokuwepo (Maasumi) basi kati yao ateuliwe anayestahiki kushikilia majukumu hayo, Mtu aliyekuwa Mwadilifu na mwenye uwezo wa kuongoza Jamii.

 1. Dalili ya Hadithi:

Marhoom Sadooq katika kitabu chake (اکمال الدين) anathibisha sapoti ya Imam Zamaan alipomjibu Ish’aaq bin Yaaqoob kwamba:

(وأمّا الحوادث الواقعة فارجعوا فيها إلی رواة حديثنا. فإنّهم حجتي عليکم وأنا حجة الله عليهم).

“Na ama matukio yanayotokea, rejeeni katika kuyatatua kwa wale wapokezi wa hadithi zetu. Kwani wao ni hoja yangu kwenu, na Mimi hoja wa Mwenyezi Mungu juu yao (kwa lile walilokufikishieni kwenu nyinyi)”.

Nini madhumuni ya neno HOJA:

 1. Sababu za hoja za Mola mlezi ziko juu ya Mja wake.
 2. Iwapo amri imekuja na Mtu akahalifu amri ile, hiyo itakuja kuwa hoja juu ya matilaba hayo (amri hiyo). Hivyo Imam ni hoja mbele ya Mungu, iwapo atasema jambo na watu wakawa hawakulitekeleza, Basi Mungu kwa maneno hayo yatakuwa ni hoja kwa waliopinga, nao hawatokuwa na udhuru wowote juu ya hilo.

Wilayatul Faqiih ni; Hoja kutoka kwa Imam, Iwapo ataamuru jambo, sawa iwe katika mlango wa Fatwa au kudadafua hukumu n.k… na watu wakahalifu basi Imam Mahdi (a.s) atakuwa dhidi ya wapinzani hao.

minajili hiyo Wilayatul Faqiih ni hoja kwa Imam kwa msingi huu.

Mwanzo wa ghaiba kubwa – mwisho maisha ya Sheikh Toosiy:

Hatua hii ilikuwa ni hatua ya mwisho wa zama za upokezi wa Hadithi na Riwaya na kuanza Hatua ya kufafanua matawi ya Dini kutoka katika Misingi ya Dini. Na wanazuoni wa wakati huo walikuwa ni:

 1. Sheikh Moofeed.
 2. Abu as-Salaah Hilliy.
 3. Sayyed Murtadhaa.
 4. Salaar Deylamiy.
 5. Sheikh Toosiy. Hatua hii ilikuwa ni kipindi cha dalili na pia akiwepo Imam Maasumi (a.s).

Nadharia za Sheikh Mufeed katika anuani ya kwanza ya Faqiih wa juu katika kipindi cha mwanzo wa Ghaiba kubwa, ilisadifiana na kuanzishwa suala la Wilayatul Faqiih. Na hapa tuashirie baadhi ya nukta, akiashiria suala la Wilayatul Faqiih:

 • Kutekeleza Adhabu za kisheria na hukumu.

Yeye anaweza kutoa adhabu za kisheria na hukumu katika wakati wa Ghaiba ya Imam Maasumi, kwani yote hayo ni katika Nyadhifa za Wanashria walio waadilifu.

(فأما إقامة الحدود فهو الی سلطان الإسلام المنصوب من قبل الله تعالی وهم أئمّة الهدی من آل محمدٍ و من نصبوه لذلک من الأمراء والحکام وقد فوّضوا النظر فيه الی فقهاء شيعتهم مع الإمکان).

 • Mwenyezi Mungu amewateua Maimam maasumina moja kwa moja kwa anuani ya viongozi wa jamii ya Kiislam na kutimiza adhabu zake.
 • Viongozi na Mahakimu kwa anuani ya Manaibu makhsusi wa Maimamu maasumina, wameteuliwa kuongoza jamii ya Kiislamu.
 • Wanachuoni wa sheria pia wameteuliwa na Maimamu kwa anuani ya kuongoza Jamii ya Kiislamu.
 • Kupigana Jihadi dhidi ya Makafiri:

Kama suala la kutekeleza adhabu na kufanyia kazi hukumu za Mungu ni katika majukumu ya Walii Faqiih, basi kupigana Jihadi na Makafiri, kuamrisha mema na kukemea mabaya ni katika mambo muhimu na majukumu ya Wanazuoni wa Dini. Kwa sababu:

Masharti ya Walii Faqiih;

 1. Uadilifu na Uchamungu.
 2. Ujuzi wa elimu ya fiq’h na hukumu za sheria ya Kiislamu.
 3. Uwezo wa Uongozi wa kuongoza Jamii.
 • Kusimamisha Sala za Ijumaa, Eid fitr na Eid Adh’haa n.k
 • Ukaadhi:

(وللفقهاء من شيعة آل محمدٍ (ص) أن يجمعوا بأخوانهم في الصلاة الجمعة وصلوات الأعياد والإستسقاء والخسوف والکسوف إذا تمکّنوا ذالک وآمنوا فيه من مضرّة اهل الفساد ولهم أن يقضوا بينهم بالحقّ ويصلحوا بين المختلفين في الدعاوی عند عدم البيّنات ويفعلوا جميع ما جعل الی القضاة في الإسلام لأنّ الأئمّة (ع) قد فوّضوا اليهم ذلک عند تمکّنهم منه بما ثبت عنهم من الأخبار وصحّ به عند أهل المعرفة من الآثار).[1]

 • Kutumia Mali ya ngawira kwa kugawia Waislamu na wasiojiweza, mayatima n.k.

(ليس لأحدٍ أن يعمل في شيئٍ ممّا عددناه من الأنفال إلّا بإذن الإمام العادل).

 • Kutumia katika Mali ya Zakat.
 • Uangalizi na matumizi wa Mali ya Mayatima.

@@ Majukumu mengine ya Walii Faqiih kwa mujibu wa nadharia ya Muhaqqiq Naraqiy:

 • Kutoa fatwa.
 • Kutoa adhabu.
 • Kusimamia mambo ya Mayatima, wendawazimu n.k
 • Kusimamia mambo ya wasiokuwepo.
 • Usimamizi wa masuala ya Ndoa.
 • Kufuatilia haki zote zinazohusiana na Mali na mengine yasiyo husiana na Mali.
 • Kutumia katika Mali za Imam (a.s).
 • Yote yaliyothibika katika Dini.
 • Mambo yasiyotakiwa kupuuziwa.

Wanazuoni waliokuwa mwanzoni wa Ghaiba kubwa ya Imam:

 • Sayyed Murtadhaa.
 • Elmul Hudaa.
 • Hamza bin Abdulaziz Deylamiy.
 • Abu Saaleh Hilliy.
 • Sheikh at-Taifah Toosiy.
 • Qaadhiy Ibn Barraaj.
 • Ibn Idriss Hilliy.

Wote hao walikizungumzia juu ya suala la Wilayatul Faqiih.

Wassalaam alaykum warahmatullah wabarakaatuh.

Imetarjumiwa na:

Juma R. Kazingati.

[1] Al Muqni’ah, cha Sheikh Mufeed, uk 811.

ارسال یک پاسخ

Barua pepe yako haitachapishwa.
Sehemu ya lazima imeonyeshwa kwa alama ya * .

*


Wasiliana nasi | RSS | Ramani ya Tovuti

Haki zote za Tovuti hii Islam 14 zimehifadhiwa,hivyo inaruhusiwa kutumia makala yoyote ya tovuti hii sambamba na kutaja chanzo chake.