Makala mpya

Dhamini kazi yetu

UADILIFU WA MASAHABA: sehemu ya 1.

adalat_sahabaSalam alaykum warahmatullah wabarakaatuh..

Tukiwa sehemu ya kwanza ya Mada yetu inayohusiana na suala la Masahaba wa Mtukufu Mtume (s.a.w).

Moja katika sababu za maadui wa Ushia wanazotumia kuakufurisha na kuhalalisha kuwaua ni suala la kwamba; Mashia huwatukana masahaba. Jambo ambalo ni Uongo na uzushi.

Awali ya yote, masahaba wakamilifu wa Mtume ni mfano wa Salman, Abuu dharr na Mikdad.

Hivyo basi tutabainisha hoja kwa kujibu tuhuma hizo za uongo.

Zipo aina mbili za itikadi kuhusu masahaba wa Mtume:

  • Wako wanaoamini kuwa masahaba wote wa Mtume ni waadilifu. Waliojitolea kwa ajili ya Dini yao, na hakuna yeyote mwenye haki ya kufuatilia hilo.

(Wanaendelea kusema kuwa, Masahaba walikuwa wakifanya ijtihad, hivyo kufanyiwa kazi fatwa zao inajuzu, hata kama wamekosea, watalipwa thawabu moja). Na yeyote hana haki ya kufuatilia hilo, na atakaye fuatilia hilo, basi huyo ni kafiri, kwanini anamjadili sahaba wa Mtume).

Kwa mujibu wa Aya hii:

لَقَدْ رَضِيَ اللَّهُ عَنِ الْمُؤْمِنينَ إِذْ يُبايِعُونَكَ تَحْتَ الشَّجَرَةِ فَعَلِمَ ما في‏ قُلُوبِهِمْ فَأَنْزَلَ السَّكينَةَ عَلَيْهِمْ وَ أَثابَهُمْ فَتْحاً قَريباً.

“Kwa hakika Mwenyezi Mungu amewapa radhi Waumini walipo fungamana nawe chini ya mti, na alijua yaliyomo nyoyoni mwao. Basi akateremsha utulivu juu yao, na akawalipa kwa Ushindi wa karibu”.

  • Nadharia ya pili: Vigezo vya Haki na Batili, Muumini na asiye Muumin, si kuwa sahaba wa Mtume wala Mke wa Mtume tu.

Bali vigezo vya Haki na Batili ni; Kama asemavyo Allah katika kitabu chake:

وَ لَقَدْ أُوحِيَ إِلَيْكَ وَ إِلَى الَّذينَ مِنْ قَبْلِكَ لَئِنْ أَشْرَكْتَ لَيَحْبَطَنَّ عَمَلُكَ وَ لَتَكُونَنَّ مِنَ الْخاسِرينَ.

“Na kwa yakini yamefunuliwa kwako na kwa walio kuwa kabla yako: Bila ya shaka ukimshirikisha Mwenyezi Mungu a’mali zako zitaanguka, na lazima utakuwa miongoni mwa wenye kukhasiri”.

Pia miongoni mwa vigezo vya Kuingia katika pepo ni mtu mwenye imani; Uchamungu, Imani na Kumfuata Mtume. Anasema Allah:

إِنَّ أَكْرَمَكُمْ عِنْدَ اللَّهِ أَتْقاكُمْ إِنَّ اللَّهَ عَليمٌ خَبيرٌ.

“Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kujua, Mwenye khabari”. Al-hujuraat; 13.

Uchamungu ni kigezo tosha cha kuwa mtu bora anayestahiki pepo, na si kuwa sahaba, kwani wapo waliokuwa wanafiki, hao pia huhesabika kuwa ni katika waadilifu? Hapana. Vile vile kuhusiana na wakeze Mtume, kama awakemeavyo Allah katika Kitabu chake kuwa;

يا نِساءَ النَّبِيِّ مَنْ يَأْتِ مِنْكُنَّ بِفاحِشَةٍ مُبَيِّنَةٍ يُضاعَفْ لَهَا الْعَذابُ ضِعْفَيْنِ وَ كانَ ذلِكَ عَلَى اللَّهِ يَسيراً.

“Enyi wake wa Nabii! Atakaye fanya uchafu dhaahiri miongoni mwenu, atazidishiwa adhabu mara mbili. Na hayo kwa Mwenyezi Mungu ni mepesi”. Ahzaab; 30.

Hivyo kuitikadia kuwa Masahaba wote wa Mtume kuwa ni waadilifu ni; Maneno yasiyokuwa na msingi wowote, si kwa dalili za kimantiki hata vile vile Historia inathibitisha hilo. Na sababu ya kushuka Suratul Munaafiqiin ni katika kukemea waliokuwa katika zama za Mtume hata katika wafuasi wake.

Pia ziko Aya nyingi na Hadithi zinazoelezea juu ya Wanafiki: kama asemavyo tena Mwenyezi Mungu mtukufu, katika surat Munafiqun;

وَمِمَّنْ حَوْلَكُمْ مِنَ الْأَعْرَابِ مُنَافِقُونَ وَمِنْ أَهْلِ الْمَدِينَةِ مَرَدُوا عَلَى النِّفَاقِ لَا تَعْلَمُهُمْ نَحْنُ نَعْلَمُهُمْ سَنُعَذِّبُهُمْ مَرَّتَينِ ثُمَّ يرَدُّونَ إِلَى عَذَابٍ عَظِيمٍ.‏

“Na katika mabedui walio jirani zenu wamo wanaafiki; na katika wenyeji wa Madina pia wapo walio bobea katika unaafiki. Wewe huwajui. Sisi tunawajua. Tutawaadhibu mara mbili, kisha watarudishwa kwenye adhabu kubwa”.

إِذا جاءَكَ الْمُنافِقُونَ قالُوا نَشْهَدُ إِنَّكَ لَرَسُولُ اللَّهِ وَ اللَّهُ يَعْلَمُ إِنَّكَ لَرَسُولُهُ وَ اللَّهُ يَشْهَدُ إِنَّ الْمُنافِقينَ لَكاذِبُونَ.

“Wanapo kujia wanaafiki husema: Tunashuhudia ya kuwa wewe ni Mtume wa Mwenyezi Mungu. Na Mwenyezi Mungu anajua kuwa wewe ni Mtume wa Mwenyezi Mungu, na Mwenyezi Mungu anashuhudia ya kuwa hakika wanaafiki ni waongo”.

Sahihi bukhari, Juz 8, uk 121.

وَقَالَ أَحْمَدُ بْنُ شَبِيبِ بْنِ سَعِيدٍ الحَبَطِيُّ، حَدَّثَنَا أَبِي، عَنْ يُونُسَ، عَنْ ابْنِ شِهَابٍ، عَنْ سَعِيدِ بْنِ المُسَيِّبِ، عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ: أَنَّهُ كَانَ يُحَدِّثُ: أَنَّ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ: ” يَرِدُ عَلَيَّ يَوْمَ القِيَامَةِ رَهْطٌ مِنْ أَصْحَابِي، فَيُحَلَّئُونَ عَنِ الحَوْضِ، فَأَقُولُ: يَا رَبِّ أَصْحَابِي، فَيَقُولُ: إِنَّكَ لاَ عِلْمَ لَكَ بِمَا أَحْدَثُوا بَعْدَكَ، إِنَّهُمُ ارْتَدُّوا عَلَى أَدْبَارِهِمْ القَهْقَرَى.

Amesema Ahmad bin Shabiib bin Said al-habatwiy, ametuhadithia Baba yangu, kutoka kwa Yunus, kutoka kwa ibn Shihaab, kutoka kwa Said bin al-mayyib, kutoka kwa Abuhuraira: Kwamba alikuwa akisema: kwamba Mtume (sww) alisema: “Yatapitishwa siku ya kiama makundi ya Masahaba wangu, wataondolewa katika Hodhi, nitasema: Ee Mola wangu! Masahaba wangu, Mungu atasema: Hakika Wewe hujui walichozua baada yako, Hakika wao wameritadi na kurejea katika mila zao potovu”.

Kwa mujibu wa Hadithi hii, suala la kufuatilia masahaba ni lazima litumike ili kubainisha ni yupi mkweli na yupi mnafiki. Yupi wa kufuatwa na yupi wa kutofuatwa. Hii ni kwa mujibu wa kauli ya Allah aliposema:

يا أَيُّهَا الَّذينَ آمَنُوا إِنْ جاءَكُمْ فاسِقٌ بِنَبَإٍ فَتَبَيَّنُوا أَنْ تُصيبُوا قَوْماً بِجَهالَةٍ فَتُصْبِحُوا عَلى‏ ما فَعَلْتُمْ نادِمينَ.

“Enyi mlio amini! Akikujieni mpotovu na khabari yoyote, ichunguzeni, msije mkawasibu watu kwa kuto jua, na mkawa tena wenye kujuta kwa mliyo yatenda”. Al-hujuraat; 6.

Suali: Tutasadiki je! Kuhusu Abuu Sufian, ambaye miaka dahari alimfanyia Mtume vitimbi? Katika vita vya washirikina na Waislamu alifanya mbinu, na yeye alipelekea vifo vya masahaba wengi wema. Mfano Hamza na wengine wengi…ambapo baada ya ufunguzi wa Makka akadhihirisha Uislamu baada ya kukosa njia ya kukimbilia.

Iweje! Ghafla awe mwenye kufuatwa kwa kauli na matendo yake?

Hivyo, Aya ya wanafiki ilimshukia Nani?

Ikiwa masahaba wote wako peponi kwa kuwa ni mujitahidiin, basi Allah atakuwa amekosea kwani, hata wanafiki atakuwa amewakusanya baina ya masahaba wema.

Je! Ipo Aya katika Qur’ani inayosema kuwa Masahaba wote ni safi na wako peponi?

Japokuwa Hadithi ya Sahihi bukhari na Aya ya Qur’an inakhalifu madai hayo.

إِنَّ الْمُنافِقينَ فِي الدَّرْكِ الْأَسْفَلِ مِنَ النَّارِ وَ لَنْ تَجِدَ لَهُمْ نَصيراً.

“Hakika wanaafiki watakuwa katika t’abaka ya chini kabisa Motoni, wala hutompata yeyote wa kuwanusuru”.

إِنَّ الَّذينَ يُبايِعُونَكَ إِنَّما يُبايِعُونَ اللَّهَ يَدُ اللَّهِ فَوْقَ أَيْديهِمْ فَمَنْ نَكَثَ فَإِنَّما يَنْكُثُ عَلى‏ نَفْسِهِ وَ مَنْ أَوْفى بِما عاهَدَ عَلَيْهُ اللَّهَ فَسَيُؤْتيهِ أَجْراً عَظيماً.

“Bila ya shaka wanao fungamana nawe, kwa hakika wanafungamana na Mwenyezi Mungu. Mkono wa Mwenyezi Mungu uko juu ya mikono yao. Basi avunjaye ahadi hizi anavunja kwa kuidhuru nafsi yake; na anaye tekeleza aliyo muahadi Mwenyezi Mungu, Mwenyezi Mungu atamlipa ujira mkubwa”.

Kwa maana kwamba kutoa kiapo cha utiifu kwa Mtume wa Allah si kigezo madhubuti, bali kigezo ni kutii na kumfuata Mtume hadi mwisho wa maisha, kusimama kidete pamoja naye katika kila hali, kwani wako miongoni mwao wametoa kiapo cha utiifu kwa unafiki, kama isema vyo Qur’ani;

وَ إِذا قيلَ لَهُمْ آمِنُوا كَما آمَنَ النَّاسُ قالُوا أَ نُؤْمِنُ كَما آمَنَ السُّفَهاءُ أَلا إِنَّهُمْ هُمُ السُّفَهاءُ وَ لكِنْ لا يَعْلَمُونَ. وَ إِذا لَقُوا الَّذينَ آمَنُوا قالُوا آمَنَّا وَ إِذا خَلَوْا إِلى‏ شَياطينِهِمْ قالُوا إِنَّا مَعَكُمْ إِنَّما نَحْنُ مُسْتَهْزِؤُنَ.

“Na wanapo ambiwa: Aminini kama walivyo amini watu. Husema: Tuamini kama walivyo amini wapumbavu? Hakika wao ndio wapumbavu, lakini hawajui tu. Na wanapo kutana na walio amini husema: Tumeamini. Na wanapo kuwa peke yao na mashet’ani wao husema: Hakika sisi tu pamoja nanyi. Hakika sisi unawadhihaki tu”.

Usikose kuwa nami katika makala ijayo…

Wassalaam alaykum warahmatullah wabarakaatuh…

Imeletwa kwenu na:

Juma R. Kazingati

ارسال یک پاسخ

Barua pepe yako haitachapishwa.
Sehemu ya lazima imeonyeshwa kwa alama ya * .

*


Wasiliana nasi | RSS | Ramani ya Tovuti

Haki zote za Tovuti hii Islam 14 zimehifadhiwa,hivyo inaruhusiwa kutumia makala yoyote ya tovuti hii sambamba na kutaja chanzo chake.