Makala mpya

Dhamini kazi yetu

UADILIFU WA mASAHABA: sehemu ya 2.

thumbnailSalaam alaykum warahmatullah wabarakaatuh..

Karibu tena katika muendelezo wa Mada yetu ya Uadilifu wa masahaba sehemu ya 2. Kama tulivyo bainisha kuwa zipo dalili nyingi zinazokanusha uadilifu wa masahaba kutoka katika Qur’ani na hadithi hata Historia zilizopokelewa kutoka pande zote mbili ambazo hazina shaka ndani yake.

Hapa tubainishe suala la kushangaza, ni kwamba, wanadai kuwa hata Mtume pia anakosea, kiasi kwamba alipewa Wahyi na Sheitani. Lakini kuhusu masahaba wanakemea vikali, kuwa hawatendi makosa. Kiasi kwamba wameshika yale waliyoharamisha Masahaba ambayo ameyahalalisha Mtume (s.a.w.w) na kuyaweka ya Mtume pembeni.

حَدَّثَنَا مَالِكِ بْنُ أَنَسٍ عَنْ نَافِعٍ عَنِ ابْنِ عُمَرَ قَالَ (قَالَ عُمَرُ مُتْعَتَانِ كَانَتَا عَلَى عَهْدِ رَسُولِ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ أَنَا أَنْهِي عَنْهُمَا وَأُعَاقِبُ عَلَيْهِمَا مُتْعَةُ النِّسَاءِ وَمُتْعَةُ الْحَجِّ). (التمهيد لما في الموطأ من المعاني والأسانيد ج10 ص113).

Ametuhadithia Malik bin Anas kutoka kwa Naaf’I kutoka kwa Ibn Omar amesema: (Amesema Omar kwamba: Mut’a mbili zilikuwa wakati wa Mjumbe wa Mwenyezi Mungu (s.a.w) mimi ninazikataza kuanzia sasa, na nitatoa adhabu kwali kwa atakayeziendeleza: Mut’a ya wanawake na Mut’at al-Hajj).

(Rejea: Attamhiid katika Al-muwatii minal-ma’aniy wal-asaanid, juz 10, uk 113).

Sasa basi, kati ya Sunna za Mtume na Sahaba, tushike zipi? Za khalifa aliyeharamisha alichokihalalisha Mtume, au tushike ya Mtume aliyotumwa na Mwenyezi Mungu mtukufu?

Swali lingine: Kundi la waliopanga njama za kumuua Othmani, je! Nao ni waadilifu? Na walichokifanya ni sahihi na watalipwa mema mbele ya Allah?

Ila Majibu yao tunakuta kwamba wanasema kuwa: Wameritadi.

Na Wale waliosimama kupambana na Imam Ali (as) katika vita vya Ngamia na Sifin na nahrawan, Je! Nao wameritadi?

Vile vile majibu yao ni kwamba; Wamefanya ijtihad katika hilo, japo wamekosea, ila hawajaritadi, ingawaje watalipwa mema kwa Mola wao.

Vita vitatu vimezuka na watu zaidi ya 150 wameuawa, wanasema waliosababisha vita hivyo kweli ni masahaba. Lakini bado tunawahesabu kuwa ni Waadilifu.

Jeneza la Imam Hassan mjukuu wa Mtume limevamiwa na kuvunjwa, na waliolivunja ni masahaba wa Mtume, je! Bado mnawahesabu kuwa ni waadilifu?.

Wamemtusi Mtume kuwa amechanganyikiwa, bado wanasema kuwa ni masahaba na ni waadilifu vile vile.

Yaazid amepelekea kifo cha Imam Hussein Mjukuu wa Mtume, wameharibu Ka’abah, wamehalalisha mji wa madina, kiasi kwamba mabinti wamepotezewa usichana wao (wamebakwa mabinti wa mji huo), bado wanasema kuwa amefanya khalifa wa Mtume.

Sawa; kwa mujibu wa fikira kama hizo, kila jambo la haramu litahalalishwa, na la halali kuharamishwa.

Sahaba ambaye amepambana sambamba na Mtume katika Jihadi mbalimbali, kiasi kwamba amefikia hatua ya kufanya njama za Kumuua Mtume huyo wa Mungu, kama isemavyo kauli ya Allah

(يَحْلِفُونَ بِاللَّهِ ما قالُوا وَ لَقَدْ قالُوا كَلِمَةَ الْكُفْرِ وَ كَفَرُوا بَعْدَ إِسْلامِهِمْ وَ هَمُّوا بِما لَمْ يَنالُوا)

Je! Huyo badoni  Muadilifu kwa maelezo ya madai yao?

Sahaba aliyekanusha amri ya Mtume baada ya kuharamishwa pombe, lakini yeye akanywa. Bado wanadai amefanya jitihada na alikuwa sahaba, bado tunamhesabu kuwa ni Muadilifu.

Khalid bin Walid, amemuua Malik bin Nuwairah, kisha akambaka mkewe Malik, bado wanadai kusema amefanya jitihada, japo ilikuwa ni makosa, lakini ni sahaba na atalipwa mema kwa Mola wake.

Ambapo khalifa wa pili alilikinza suala hilo, kiasi kwamba akatia dosari kitendo hicho, na kutoa ombi Khalid aadhibiwe, lakini Khalifa wa kwanza alikataa Khalid asiadhibiwe.

Swali: Je! Malik si sahaba, kiasi kwamba afanyiwe madhila kama hayo.

Waliomuua Othman, hawakuwa masahaba.

Abdillah bin Salul, aliyehukumiwa kifo na Mtume, hakuwa sahaba.

Pia, katika umma zilizotanguliwa mfano Qaroon, samiriy, Yahooda eskariato, walikuwa ni miongoni mwa wafuasi wa Manabii, ila walikuwa ni katika wanafiki. Walijikurubisha kwa Mitume ili kutia dosari na dharuba katika Dini za manabii hao na hatimae kuwadhuru.

  • Qur’ani inasimulia Msimamo wa masahaba katika vita vya Hunaini, Allah anasema;

إِنَّ الَّذينَ تَوَلَّوْا مِنْكُمْ يَوْمَ الْتَقَى الْجَمْعانِ إِنَّمَا اسْتَزَلَّهُمُ الشَّيْطانُ بِبَعْضِ ما كَسَبُوا وَ لَقَدْ عَفَا اللَّهُ عَنْهُمْ إِنَّ اللَّهَ غَفُورٌ حَليمٌ.

“Hakika wale walio rudi nyuma miongoni mwenu siku yalipo pambana majeshi mawili, Shet’ani ndiye aliye watelezesha kwa sababu ya baadhi ya makosa waliyo yafanya; na Mwenyezi Mungu amekwisha wasamehe. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusamehe, Mpole”.

  • Kumbeza Mtume wakati wa kugawa sadaka;

وَ مِنْهُمْ مَنْ يَلْمِزُكَ فِي الصَّدَقاتِ فَإِنْ أُعْطُوا مِنْها رَضُوا وَ إِنْ لَمْ يُعْطَوْا مِنْها إِذا هُمْ يَسْخَطُونَ.

“Na miongoni mwao wapo wanao kusengenya katika kugawa sadaka. Wanapo pewa wao huridhika. Na wakito pewa hukasirika”.

  • Wanafiki waliokando ya Mtume;

وَ مِمَّنْ حَوْلَكُمْ مِنَ الْأَعْرابِ مُنافِقُونَ وَ مِنْ أَهْلِ الْمَدينَةِ مَرَدُوا عَلَى النِّفاقِ لا تَعْلَمُهُمْ نَحْنُ نَعْلَمُهُمْ سَنُعَذِّبُهُمْ مَرَّتَيْنِ ثُمَّ يُرَدُّونَ إِلى‏ عَذابٍ عَظيمٍ.

“Na katika mabedui walio jirani zenu wamo wanaafiki; na katika wenyeji wa Madina pia wapo walio bobea katika unaafiki. Wewe huwajui. Sisi tunawajua. Tutawaadhibu mara mbili, kisha watarudishwa kwenye adhabu kubwa”.

  • Waongo miongoni mwao kwa lengo la kukimbia Vita;

يَسْتَأْذِنُ فَريقٌ مِنْهُمُ النَّبِيَّ يَقُولُونَ إِنَّ بُيُوتَنا عَوْرَةٌ وَ ما هِيَ بِعَوْرَةٍ إِنْ يُريدُونَ إِلاَّ فِراراً.

“Na kundi jingine miongoni mwao likaomba ruhusa kwa Mtume kwa kusema: Hakika nyumba zetu ni tupu. Wala hazikuwa tupu; hawakutaka ila kukimbia tu”.

  • Kwa fikira kama hizo, imepelekea Banii Umayya kutawala zaidi miaka sabini, na kumlaani Imam Ali kwenye majukwaa misikitini.

Hivyo, kwa maelezo haya, ni kwamba yatupasa kuzirejea Aya na Hadithi, pia Historia ili kugundua ni sahaba yupi mkweli na yupi mnafiki, muislamu wa kweli na mbabaishaji…

Tamati.

Imeletwa kwenu na:

Juma R. Kazingati

ارسال یک پاسخ

Barua pepe yako haitachapishwa.
Sehemu ya lazima imeonyeshwa kwa alama ya * .

*


Wasiliana nasi | RSS | Ramani ya Tovuti

Haki zote za Tovuti hii Islam 14 zimehifadhiwa,hivyo inaruhusiwa kutumia makala yoyote ya tovuti hii sambamba na kutaja chanzo chake.