Makala mpya

Dhamini kazi yetu

TAWASSUL: Sehemu ya 1

a1Salaam alaykum warahmatullah wabarakaatuh…

 • Kulingana na matukio yote yanayotokea Ulimwenguni, na miongoni mwa dalili zake ni Kukufurishana n.k wako wanaodai kuwa ni kwa sababu ya Kufanya: Tawassal kwenye makaburi ni shirki…

Nukta ni kwamba:

 • Kila dhehebu katika madhehebu ya Shia na Sunni wanayo mahala pa ziara (Kama kaburi la Abu hanifa).
 • Kuomba msaada kupitia Mashahidi, ni kwa sababu wao wako Hai (Hivyo kukufurisha watu wanaofanya hivyo ni kwenda kinyume na Qur’ani Surat Maida Aya 105).
 • Muhammad Kitaaniy mwandishi wa kisalafi, anaunga mkono kuwa maisha ya Mtume (s.a.w.w) ni bora kuliko viumbe wote. Kama vile kutoa salamu katika Sala…

(Je! Salam hii ni ya bure, haina thamani yoyote?) tambua kuwa Mtume wa Mungu anaona matendo yetu yote).

Mfano mwengine ni pale wana wa Israeli walipomuomba Nabii Yaakub kuwaombea msamaha kwa Mwenyezi Mungu, je! Hiyo pia ni shirk?

 • Majibu ya madai ya kufanya tawassal kwa waliokufa kuwa ni Shirk

(السلام علیک أيها النبي ورحمة الله وبرکاته)

 • Wafu wote waliokufa katika njia ya M/Mwenyezi wako Hai.
 • M/Mungu huwazumgumzia walokufa katika Surat Baqarah Aya 150, na kwamba hawajafa.
 • Surat Aali Imran Aya 159, inasema kuwa wafu wote wako mbele ya Mola wao. Sasa Mwenyezi Mungu yuko wapi?

(Popote muelezako Nyuso zenu, basi huko yupo Mola wenu). (Sasa basi popote muelekepo nyuso zenu, basi na Mashahidi waliokufa katika Njia ya Mola wao wapo kila sehemu).

(Surat Mumtahinah 13, M/Mungu anasema: Hakika tumekutuma ili uwe ni shahidi kwao).

Sasa basi, kuwakufurisha wanaozuru makaburi ya waja wema ni mahala pake? Na hiyo ni kwa madai kwamba: Aliyekwisha kufa ameondoka.

Hivyo kwa mujibu wa Aya hizo, zinajuzisha kusimama juu ya makaburi ya Waja wema na kuomba msaada kupitia wao.

 • Tofauti kati ya Muumini na Kafiri:
 1. Muamini huitakidia kuwa, Kifo ni hatua nyingine baada ya maisha ya Duniani, pia ni mwanzo maisha mapya baada ya Dunia hii.
 2. Kafiri huitikadia kuwa, baada ya maisha haya hakuna maisha mengine baadae.

Katika makala ijayo tutazungumzia Tawassal kwa mujibu wa Hadithi za Ahl Sunna…

Usikose kuwa nami katika makala ijayo..

Wassalam alaykum warahmatullah wabarakaatuh…

Imeandaliwa na:

Juma R. Kazingati.

ارسال یک پاسخ

Barua pepe yako haitachapishwa.
Sehemu ya lazima imeonyeshwa kwa alama ya * .

*


Wasiliana nasi | RSS | Ramani ya Tovuti

Haki zote za Tovuti hii Islam 14 zimehifadhiwa,hivyo inaruhusiwa kutumia makala yoyote ya tovuti hii sambamba na kutaja chanzo chake.