Makala mpya

Dhamini kazi yetu

UHARAMU WA PUNYETO.

estemnaUHARAMU WA PUNYETO.

Kujikimu mahitaji ya kijinsia kwa kutumia njia mbalimbali na kutoa manii ni jambo tumekwisha lizungumzia hapo mwanzo kuwa ni miongoni mwa madhambi makubwa, jambo ambalo Uislamu umelipiga vita.

Hivyo basi ni lazima ifahamike kwamba punyeto ni sawa na mtu kujioa yeye mwenyewe kwa kumwaga maji ya uzazi kutumia mkono, ambapo kitendo hicho kimegawanyika katika aina kadhaa; Mfano kujichezea kwa mkono. Kusikiliza maongezi au sauti za Wanawake ajnabi kiasi kwamba ikapelekea kufanya kitendo hicho. Kujadiliana kuhusiana na maswala ya kimapenzi. Kuvuta taswira yale yanayosisimua hisia za matamanio ya kijinsia. Hivyo yeyote atakayekusudia kutenda kitendo cha kutoa manii kwa mkono kwa hiari yake mwenyewe, basi atakuwa ametenda dhambi kubwa ambayo kwa mujibu wa Dini tukufu ya Kiislamu ni haramu.

UHARAMU WA PUNYETO KWA MUJIBU WA QUR’ANI

“وَ الَّذِينَ هُمْ لِفُرُوجِهِمْ حافِظُونَ إِلَّا عَلى‏ أَزْواجِهِمْ أَوْ ما مَلَكَتْ أَيْمانُهُمْ فَإِنَّهُمْ غَيْرُ مَلُومِينَ فَمَنِ ابْتَغى‏ وَراءَ ذلِكَ فَأُولئِكَ هُمُ العادُون‏”.

“Na ambao wanazilinda tupu zao, Isipo kuwa kwa wake zao au kwa iliyo wamiliki mikono yao ya kulia. Kwani hao si wenye kulaumiwa. Lakini anaye taka kinyume cha haya, basi hao ndio warukao mipaka”.

Wanazuoni wa Kishia na Kisunni wamekubaliana kwa kutegemea Kitabu cha Mwenyezi Mungu ya kwamba Aya za Qur’ani zimemaanisha kulinda tupu, pamoja na kila aina inayofaa itakayoshamili suala la kitendo cha kijinsia. Vile vile imakusanya suala la Ndoa. Minajili hiyo; Wanaojihusisha na kitendo cha kulawiti, kuchezea wanawake wasiokuwa halali kwao vimekemewa vikali katika Suratul Muuminun, Aya ya 5, 6, 7. Na Suratul Ma’arij, Aya ya 29, 30 na 31.

Ikiwa itasemekana kwamba: Madhumuni ya Aya hii ni kosa kwa wale wanaomiliki Wajakazi, na wanastahiki kulaumiwa, ambapo lawama haikula kwa maana ya haramu.

Kwa hiyo lawabu ni kwamba; Katika Aya ya baadaye watu hao waliotajwa katika Aya hii kuwa ni: (Wale warukao mipaka) imetafsiriwa kuwa ni hao hao na ni madhalimu pia.

UHARAMU WA PUNYETO KWA MUJIBU WA RIWAYA

Zimepokelewa Riwaya nyingi kutoka kwa Ahlul-bayt (as) kuhusiana na matilaba haya ambayo upokezi wake hupatikana katika Kitabu Al wasail katika juzuu ya 14 mlango 28 (Annikahul Muharram) النکاح المحرم. Na juzuu ya 18 mlango wa 3, نکاح البهائم و وطی الاموات و الاستمناء (Nikaahul Bahaaim. Wat’ul amwaat. Al istimnaa’i). Ambapo miongoni mwa milango hiyo mlango unaohusiana na mada yetu umebainishwa kwa upana zaidi. Hivyo kwa maelezo zaidi rejea kitabu hicho, ili ujisomee zaidi.

TUFANYE NINI ILI TUEPUKE KITENDO HICHI CHA punyeto…!

Ikiwa mtu atalalamika kuwepo mke wake mbali naye kwa muda zaidi ya mwaka mmoja, kiasi kwamba akakosa uwezo wa kuonana naye, jambo ambalo litampa wasiwasi wa hali hiyo kuendelea zaidi ya miaka kadhaa ambapo wakati mwengine hushambuliwa na matamanio makali na hatimaye kutenda kitendo hicho, ambavyo pia suala hilo pia humtokea mkewe, lakini kila baada ya kufanya hivyo hujihisi huzuni kubwa mno na kwamba ametenda dhambi. Je ni njia ipi itakayomwezesha mtu huyo kuepukana na kutenda dhambi hiyo?

 Jawabu ni kwamba: Ni lazima mtu kama huyo atambue ya kwamba suala la kujitosheleza mwenyewe kimatamanio, ni miongoni mwa madhambi makubwa yaliyokemewa vikali na Dini tukufu ya Kiislamu, na kwamba malipo yake ni mazito mno siku ya kiama.

Hivyo njia bora ya kuepukana na kitendo hicho, ni kuoa ndoa ya kisheria (Ima ndoa ya daima au ya muda) kulingana na masharti maalumu yaliyokwisha bainishwa na wanazuoni mbalimbali juu ya suala hilo. Na njia bora ya uwokovu kwa wale waliokwisha oa, yawapasa wajiepushe kutengana na wake zao kwa muda mrefu utakaowazuia kuonana, kusafiri masafa mafupi kwa muda mfupi, ili kuepukana na mzizi wa dhambi hii kubwa na madhambi mengine makubwa. Na ikiwa itajitokeza hali ambayo itapelekea kukosekana uwezekano huo basi njia nyingine bora za kujiepusha na dhambi hii ni hizi zifuatazo kwa kumtegemea Mwenyezi Mungu amuezeshe kuzitekeleza ipasavyo:

 1. Kuchukuwa maamuzi thabiti ya kuacha kitendo hicho.
 2. Kujiepusha kutazama aina ya picha au Movie zenye kusisimua hisia za matamanio (Picha za ngono).
 3. Kuwa makini wakati wa kuteua rafiki, wasioshawishi kufanya kitendo hicho. Vile vile kuepuka kuteua marafiki wa kike (Ajnabi).
 4. Kujiepusha kuwazawaza sana, pia kujihimiza kujishughulisha na kazi zenye manufaa. Kumbuka; Kutojishughulisha, ni suala ambalo linaweza kukupelekea haraka kutenda kila kita baya.
 5. Katika hali iwezekanayo jiepusheni kukaa mahali wapweke.
 6. Kufunga (sunna) ili kudhibiti hisia za nafsi na pia ni muhimu katika kuzidhatiti hisia zako.

Ikiwa hutaweza kufunga, basi jitahidi kutokulakula sana au wakati wa kulala jiepusheni kulala ilihali tumbo limejaa kupita kiasi.

 1. Jiepusheni kula chakula chenye kuleta hisia za kijinsia, mfano; Chocholate, Strowberry, tende, vitunguu, pilipili, mayai ya kuku, nyama nyekundu, chakula chenye mafuta mengi na kadhalika…
 2. Daima usilale ukiwa ni mwenye haja ndogo.
 3. Jisomeeni usiku wakati wa kulala, pia msilalie matumbo.
 4. Jiepusheni kwa kadri iwezekanayo kuongea zaidi pamoja na watu ajnabi katika mazingira ya kazini hata familia zisizokuwa familia zenu.
 5. Jiliwazeni kwa kusoma Qur’ani pamoja na kufanya dhikri kwa wingi, kwani kumtaja Mwenyezi Mungu hutulia nafsi ya mwanadamu.

Nukta muhimu ya kuweza kukamilisha zoezi hili, ni kumtumainia Mwenyezi Mungu pamoja kumuomba msaada na kutawakkal kwake. Azimio thabiti ni njia pekee ya mafaniko ya kupambana na hisia hizo kama tulivyobainisha hapo juu. Nasi ni matumaini yetu ya kwamba kwa kutarajia hisani ya Mwenyezi Mungu mtukugu, mtaweza kupambana na hisia hizo na kuzishinda kwa ushindi mkubwa.

Dalili na madhara ya Punyeto kiMwili

 1. Maumivu ya kichwa.
 2. Uchovu na udhaifu wa viungo.
 3. Aleji na udhaifu katika sekta za mishipa.
 4. Kuitingisha
 5. Kudhoofika nguvu ya macho na kuhisi mvumo masikioni kama Nzi.
 6. Mvumo wa masikio na kuhisi kelele.
 7. Mabadiliko ya fomula ya Uso na Mwili.
 8. Kunyonyoka Nywele.
 9. Maumivu ya kiuno.
 10. Kukonda (Kupungua nyama za mwilini).
 11. Maumivu ya kiwiko cha mguu na mivupa jirani.
 12. Ukosefu wa kunawili mwili ujanani.

13.     Upungufu wa Damu (Poverty Hematology) na maumivu kufika kwenye uti wa mgongo.

 1. Udhaifu wa kumbukumbu.
 2. Kupungua korodani.
 3. Maumivu katika kuta za paja na kando ya sehemu za siri.
 4. Kushusha haraka wakati wa tendo.
 5. Kushusha bila mpangilio.
 6. Kuchelewa kuinuka.
 7. Kulala haraka.

Imeletwa kwenu na:

Juma R. Kazingati.

ارسال یک پاسخ

Barua pepe yako haitachapishwa.
Sehemu ya lazima imeonyeshwa kwa alama ya * .

*


Wasiliana nasi | RSS | Ramani ya Tovuti

Haki zote za Tovuti hii Islam 14 zimehifadhiwa,hivyo inaruhusiwa kutumia makala yoyote ya tovuti hii sambamba na kutaja chanzo chake.